Wanafunzi wa vyuo vikuu Ufaransa wajawa na ghadhabu baada ya mwanafunzi mmoja kujichoma moto
(last modified Wed, 13 Nov 2019 08:21:04 GMT )
Nov 13, 2019 08:21 UTC
  • Wanafunzi wa vyuo vikuu Ufaransa wajawa na ghadhabu baada ya mwanafunzi mmoja kujichoma moto

Kitendo cha mawanafunzi mmoja wa chuo kikuu cha Lyon nchini Ufaransa kujichoma moto na upuuzaji wa serikali ya Rais Emmanuel Macron kuhusiana na tukio hilo, kimewaghadhibisha mno wanafunzi wa vyuo vikuu wa nchi hiyo.

Hii ni katika hali ambayo François Hollande, rais wa zamani wa Ufaransa alikuwa amepanga kuhutubia jioni ya jana katika mji wa Lyon, kaskazini mwa nchi kuhusiana na mgogoro wa kidemokrasia, ambapo mamia ya wanafunzi wa chuo kikuu wenye hasira kali walivamia mkutano wake na kupelekea kuahirishwa. Kadhalika wanafunzi wengine ambao walikuwa wamepiga kambi mbele ya Wizara ya Elimu ya Juu ya Ufaransa mjini Paris walivunja uzio na kuingia katika eneo la wazi la wizara hiyo na kusababisha hasara za mali. Polisi wamewatia mbaroni makumi ya wanafunzi kadhaa.

Ghasia nchini Ufaransa

Kufuatia kujichoma moto mwanafunzi wa chuo kikuu mjini Lyon, Umoja wa Mshikamano wa Wanafunzi nchini Ufaransa jana uliitisha maandamano makubwa mbele ya vituo vya athari ya kielimu na chuo kikuu cha Crous kulalamikia hali mbaya ya maisha nchini humo. Mwanafunzi huyo aliyejeruhiwa sana na moto aliandika barua kwa ajili ya ndugu zake akisema kuwa amechukua hatua hiyo kutokana na hali ngumu ya kifedha na kulalamikia siasa mbovu za Rais Emmanuel Macron pamoja na Umoja wa Ulaya. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibu zilizotolewa na taasisi ya Odoxa, thheluthi tatu ya raia wa Ufaransa hawaridhishwi na utendaji kazi wa Rais Emmanuel Macron.

Tags