Wamarekani waunga mkono mpango wa kumshtaki Trump ICC
https://parstoday.ir/sw/news/world-i58737-wamarekani_waunga_mkono_mpango_wa_kumshtaki_trump_icc
Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani unaonesha Wamarekani wanaunga mkono mpango wa kushtakiwa rais wa nchi hiyo, Donald Trump kwa kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 25, 2020 08:09 UTC
  • Wamarekani waunga mkono mpango wa kumshtaki Trump ICC

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani unaonesha Wamarekani wanaunga mkono mpango wa kushtakiwa rais wa nchi hiyo, Donald Trump kwa kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani.

Uchunguzi wa maoni uliofanywa na mtandao wa Business Insider wa Marekani baada ya Donald Trump kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH unaonesha kuwa, zaidi ya robo ya Wamarekani wanaamini kuwa, inabidi Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC inapaswa kufuatilia kesi dhidi ya Trump kuhusiana na mauaji hayo.

Karibu asilimia 27 ya watu elfu moja na 83 walioshiriki kwenye uchunguzi huo wa maoni wamesema kuwa, wanakubaliana na Iran kwamba lazima Trump apandishwe kizimbani huko The Hague, Uholanzi.

Shahid Luteni Jenerali Qassem Soleimani

 

Mtandao huo wa Business Insider wa nchini Marekani vile vile umesema, kwa mtazamo wa wataalamu wa kimataifa, kuuliwa kigaidi Luteni Jenerali Soleimani ni shambulio la kustaajabisha mno kuwahi kufanywa na serikali ya kigeni kama Marekani na halijawahi kutokea mfano wake tangu baada ya Vita vya Pili vya Dunia.

Mivutano baina ya Marekani na Iran imeongezeka baada ya Trump kutangaza kuitoa Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA tarehe 8 Mei 2018 na kuirejeshea Iran vikwazo vyote vilivyokuwa vimeondolewa baada ya makubaliano hayo yenye baraka zote za Umoja wa Mataifa.

Tangu wakati huo hadi hivi sasa, Marekani imekuwa ikifanya ugaidi wa kiuchumi na kijeshi dhidi ya Iran, huku tukio la karibuni kabisa likiwa ni la kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH tarehe 3 mwezi huu wa Januari 2020.