Feb 11, 2020 06:59 UTC
  • Pentagon: Askari 109 wa Marekani walipatwa na ugonjwa wa ubongo katika shambulizi la makombora la Iran

Ikiwa ni katika mwenendelezo wa kukiri juu ya ongezeko la idadi ya askari magaidi wa Marekani waliojeruhiwa katika shambulizi la makombora la Iran kwenye kambi ya jeshi la Marekani ya Ain Assad nchini Iraq, Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon imetangaza kuwa askari 109 wa nchi hiyo wamekumbwa na ugonjwa wa ubongo kutokana na shambulizi hilo.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani Jumanne ya leo imesema kuwa, askari 109 wa nchi hiyo wamepatiwa matibabu kutokana na matatizo ya ubongo, ambapo wameongezeka askari 59 kwenye idadi ya awali. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Pentagon, askari 76 wamepatiwa matibabu na kurejea mahala pao pa kazi. Imeendelea kufafanua kuwa askari 75 miongoni mwao wamepatiwa matibabu nchini Iraq, huku mmoja akitibiwa nchini Ujerumani. Katika kutekeleza ahadi yake ya kulipiza kisasi kikali kwa Marekani kutokana na nchi hiyo kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na shakhsia wengine aliokuwa nao, Iran ilishambulia kwa makombora kambi ya kijeshi ya askari gaidi wa Marekani ya Ain Assad nchini Iraq hapo tarehe 8 Januari mwaka huu.

Kambi ya Ain Assad ya Marekani nchini Iraq baada ya kushambuliwa na Iran

Licha ya Trump kudai kuwa katika shambulizi hilo hakuna askari aliyeuawa wala kujeruhiwa, lakini Washington imeendelea kukiri taratibu juu ya askari wake wengi kujeruhiwa. Katika uwanja huo awali Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo ilikiri kuwa jumla ya askari 50 walijeruhiwa katika ulipizaji kisasi huo wa Iran kwenye kambi ya kijeshi ya Ain Assad. Taarifa mpya inaonyesha kuwa kinyume na madai ya awali ya Trump si tu kwamba kuna askari waliojeruhiwa, bali ni kwamba idadi ya askari hao waliojeruhiwa inazidi kuongeza.

Tags