IMF kuzisaidia nchi 28 maskini kutokana na athari mbaya za corona, nyingi ni za Afrika
(last modified 2020-10-06T11:20:00+00:00 )
Oct 06, 2020 11:20 UTC
  • IMF kuzisaidia nchi 28 maskini kutokana na athari mbaya za corona, nyingi ni za Afrika

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) umeafiki kutoa msaada wa haraka kwa nchi 28 maskini duniani kwa lengo la kupunguza madeni ya nchi hizo na kukabiliana na athari mbaya za maambukizi ya virusi vya corona.

Msaada huo unatolewa kwa lengo la kusahilisha malipo ya madeni ya nchi hizo katika kipindi cha miezi sita ijayo na kuziwezesha kutumia mapatano yao duni kwa ajili ya kuchukua hatua za dharura za matibabu na kukabiliana na janga la maambukizi ya virusi vya corona. 

Nchi nyingi zitakazofaidika na msaada huo wa IMF ni za bara la Afrika zikiwemo Tanzania, Rwanda, Gambia, Comoro. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji, Ethiopia, Burundi, Madagascar, Niger na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Msaada huo wa IMF kwa nchi 28 maskini duniani utadhaminiwa na mfuko wa kukabiliana na majanga wa IMF (fonds fiduciaire ARC).

Fedha hizo zinazokadiriwa kuwa milioni 959 zinatolewa kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya kimaumbile au masuala ya tiba na afya na zitaendelea kutolewa kwa nchi husika kwa kipindi cha miaka miwili. 

Maambukizi ya virusi vya corona yameathiri sana uchumi wa dunia na kukwamisha mipango ya ustawi na maendeleo hususan katika nchi maskini na zinazoendelea. 

Tags