Korea ya Kaskazini yakosoa hali ya haki za binadamu katika nchi za Magharibi
(last modified Tue, 23 Mar 2021 07:40:30 GMT )
Mar 23, 2021 07:40 UTC
  • Korea ya Kaskazini yakosoa hali ya haki za binadamu katika nchi za Magharibi

Korea ya Kaskazini imezikosoa nchi za Magharibi kwa kukiuka haki za binadamu na kuitolea mwito jamii ya kimataifa kuchukua hatua ya kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.

Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya Russia Today, ripoti iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Korea ya Kaskazini imeashiria ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na nchi za Magharibi na kueleza kwamba, hivi sasa katika nchi hizo raia wamekuwa wahanga wa utumiaji wa silaha moto na baridi huku makundi ya wahalifu yakiwa ndiyo yenye udhibiti wa jamii za nchi hizo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vitendo vya ukatili vinavyofanywa dhidi ya wanawake katika nchi za Magharibi vimefikia kiwango hatari kisichoweza kuelezeka.

Katika ripoti yake hiyo, wizara ya mambo ya nje ya Korea ya Kaskazini imegusia pia ubaguzi wa rangi katika Ulimwengu wa Magharibi na kuongeza kwamba, nchi za Magharibi zinapitisha sheria za kiounevu kwa kutumia kisingizio cha kutetea haki za binadamu na kueneza vipimo vya kiundumakuwili katika jamii ya kimataifa.../

Tags