Jeshi la Marekani linachoma mada ya sumu katika jamii za watu maskini zaidi nchini humo
(last modified Mon, 29 Mar 2021 04:28:19 GMT )
Mar 29, 2021 04:28 UTC
  • Jeshi la Marekani linachoma mada ya  sumu katika jamii za watu maskini zaidi nchini humo

Jeshi la Marekani linachoma kwa siri mada moja ya kemikali ya sumu hatari kwa mwanadamu karibu na jamii za watu maskini zaidi nchini humo kwa lengo la kuziangamiza jamii hizo.

Gazeti la The Guardian linalochapishwa nchini Uingereza limeripoti kuwa, jeshi la Marekani kati ya mwaka 2016 hadi mwaka jana 2020 liliamuru kuchomwa moto kwa siri zaidi ya pauni milioni 20 za mada hiyo ya sumu. Mada hiyo ya kemikali ya sumu ni ile ambayo hutumiwa na idara ya zima moto kukabiliana na matukio mbalimbali ya moto.   

Ukweli ni kuwa, kitendo cha kuichoma mada hiyo ya sumu kinasababisha kuenea sumu angani, mashambani na katika maji yanayotumiwa na watu wanaoishi kwenye maeneo hayo. 

Gazeti la The Guardian limeongeza kuwa, Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) inafanya majaribio hayo ya kemikali huku usalama na afya ya mamilioni ya raia wa nchi hiyo ikiwa hatarini kufuatia hatua hiyo. Mada hiyo ya sumu kwa jina la Aqueous Film Forming Foam (AFFF) imetengenezwa na vikosi vya ulinzi vya Marekani.  

Mada  hiyo ya kemikali ya sumu ya AFFF ilitumiwa pia katika vita vya Vietnam kwa ajili ya kuzima moto uliosababishwa na mafuta katika manowari za kivita na katika viwanja vya ndege vya kijeshi.  

Mada ya sumu inayochomwa katika jamii za watu maskini zaidi nchini Marekani

Mada hiyo ya sumu imemulikwa na kuzingatiwa pakubwa kimataifa kutokana na taathira na uharibifu mkubwa unaosababisha kwa mazingira.  

Tags