Syria: Silaha za kemikali ni mbinu pekee ya Aal-Saud kwa ajili ya kuwaokoa magaidi
(last modified Tue, 10 Apr 2018 02:48:57 GMT )
Apr 10, 2018 02:48 UTC
  • Syria: Silaha za kemikali ni mbinu pekee ya Aal-Saud kwa ajili ya kuwaokoa magaidi

Afisa mmoja wa ngazi ya juu katika serikali ya Syria amesema kuwa, utawala wa Aal-Saud unalituhumu jeshi la Syria kwamba limetumia silaha za kemikali nchini humo kwa lengo la kuwaokoa magaidi wa Kiwahabi wa Jaishul-Islami.

Afisa huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake ameyasema hayo wakati akizungumza na Shirika la Habari la Syria SANA ambapo amesisitiza kwamba, umefika wakati kwa utawala wa Aal-Saud ukomeshe uungaji mkono wake kwa magaidi wanaofanya jinai nchini Syria na katika maeneo mengine ya dunia.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria ambayo imefichua njama chafu za maadui wa Uislamu na nchi hiyo

Ameongeza kuwa hivi sasa dunia nzima inatambua nafasi hasi ya utawala huo wa Aal-Saud katika kulea na kuunga mkono makundi ya ukufurishaji na ya kigaidi nchini Afghanistan, Syria, Iraq na maeneo mengine ya dunia. Kadhalika afisa huyo wa ngazi ya juu katika serikali ya Syria amesisitiza kwamba, hii leo matatizo yote yanayowapata watu wa mataifa ya Mashariki ya Kati, ni matokeo ya siasa mbovu za utawala wa Aal-Saud na idolojia shirikishi za Saudia na makundi ya Kiwahabi. Kadhalika amefafanua kuwa, magaidi wa eneo la Ghouta Mashariki wa genge la Jaishul-wametoa pendekezo la kufanya mazungumzo na serikali baada ya kuona maji yamewafika kooni.

Wanachama wa genge la kigaidi wanaopata misaada ya kifedha kutoka Saudia na washirika wake

Hii ni katika hali ambayo madola ya Maghaibi yameendelea kutoa tuhuma dhidi ya serikali ya Rais Bashar al-Assad wa Syria kuhusiana na kadhia ya shambulizi hewa la silaha za kemikali katika mji wa Duma, ambapo katika uwanja huo imeelezwa kuwa kongresi ya Marekani inafanya njama za kumshawishi Rais Donald Trump kufanya shambulizi dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Tags