Watu 19 wafariki dunia katika moto mkubwa New York, Marekani
(last modified 2022-01-10T03:25:31+00:00 )
Jan 10, 2022 03:25 UTC
  • Watu 19 wafariki dunia katika moto mkubwa New York, Marekani

Watu wasiopungua 19 wamefariki dunia, wakiwemo watoto tisa, na makumi ya wengine kujeruhiwa katika moto uliotokea kwenye jengo la ghorofa katika jiji la New York, nchini Marekani.

Meya wa Jiji la New York, Eric Adams amethibitisha kuwa watu 19 wamefariki dunia katika moto huo uliozuka mwendo wa saa tano asubuhi siku ya Jumapili ya jana katika jengo la Twin Parks katika eneo la Bronx jijini humo. Ripoti zinasema watu wasiopungua 60 wamejeruhiwa katika moto huo na kwamba hali za baadhi yao ni mbaya sana. 

Jenge hilo lenye ghorofa 19 lina nyumba za bei nafuu na lina jamii kubwa ya watu wenye asili ya Gambia. 

Maafisa wa New York wanasema, moto huo ulianzia kwenye hita ya umeme katika chumba cha kulala cha moja ya vyumba vya jengo hilo.

19 wameaga dunia, 60 wamejerujiwa katika moto wa New York

Meya wa jiji la New York, Eric Adams amesema kuwa, moto huo ni miongoni mwa ajali mbaya zaidi za moto katika historia ya mji huo.

Moto huo ni wa pili kutokea katika majengo ya makazi ya umma nchini Marekani katika muda wa wiki moja na umezua maswali mengi kuhusu viwango vya usalama vya majengo kama hayo. 

Tags