Picha gani ni ya kweli?
Parstoday- Mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X amefanya ulinganishaji kati ya filamu ya The Pianist (Mpiga Piano) na mandhari ya malalamiko na upinzani ya Mkuu wa Hospitali ya Kamal Adwan huko Gaza.
Elias, mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X, aliweka picha za filamu ya Hollywood ya "The Pianist" na Dk Hussam Abu Safiya Mkuu wa Hospitali ya Kamal Adwan huko Gaza na kuandika kwenye mtandao huu wa kijamii: "Moja ni filamu na moja ni halisi."
Ulinganishaji filamu maarufu ya "The Pianist" na mandhari ya malalamiko ya Mkuu wa Hospitali "Kamal Adwan"
Kulingana na Parstoday, filamu ya The Pianist (Mpiga Piano) ilitengenezwa na Roman Polanski mwaka wa 2002 na ni maelezo ya wazi ya maisha yaliyokandamizwa ya Wayahudi wakati wa Vita Kuu ya II. Katika upande mwingine, picha za Dakta "Hussam Abu Safiya" akionyesha malalamiko yake mbele ya vifaru vya utawala ghasibu wa Kizayuni huko kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza ni taswira halisi ya ukandamizaji wa wananchi wa Palestina na jinai za utawala ghasibu wa Israel. .

Mmoja wa maafisa wa jeshi la utawala ghasibu wa Israel amekiri katika mazungumzo yake na kanali ya ABC ya Marekani kwamba "Hussam Abu Safiya", Mkurugenzi Mkuuu wa hospitali ya "Kamal Adwan" amekamatwa na utawala wa Kizayuni. Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umetaka kuachiliwa kwake na kuacha kulenga vituo vya matibabu huko Gaza.
Idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi tangu kuanza hujuma kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Gaza (Oktoba 7, 2023) inaelezwa kuwa imekaribia watu 46,000.
Uungaji mkono wa wazi wa Marekani na nchi za Magharibi umepelekea kushuhudiwa faili jeusi la viongozi watenda jinai wa utawala wa Kizayuni wanaoua watu wasio na ulinzi wala hatia. Bila shaka wale wote wanaohami na kuunga mkono jinai za Israel wanahusika pia katika jinai na mauaji ya kimbari ya utawala huo katika Ukanda wa Gaza.