Sep 25, 2017 07:21 UTC
  • Boko Haram 1600 kufikishwa mahakamani Oktoba, Nigeria

Wizara ya Sheria ya Nigeria imetangaza kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haram wanaoshikiliwa katika korokoro za nchi hiyo watafikishwa mahakamani Oktoba mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Sheria ya Nigeria imesema kuwa, maandalizi yote ya kufikishwa mahakamani watuhumiwa hao yamekamilika na mawakili wao wataainishwa hivi karibuni. 

Wakati huo huo jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, maelfu ya watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haram wanashikiliwa katika magereza za nchi hiyo na kwamba wengi wao hawajafikishwa mahakamani. Taarifa ya vyombo vya usalama vya Nigeria inasema kucheleweshwa kwa kesi za washukiwa hao kunatokana na matatizo ya vitendea kazi.

Maiti za raia waliouawa katika shambulizi la Boko Haram, Nigeria

Maelfu ya watu wameuawa na mamilioni ya wengine kukimbia makazi yao hususan huko kaskazini mwa Nigeria kutokana na mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi. 

Tags