Nov 26, 2017 03:45 UTC
  • Wanigeria waandamana kutaka Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu aachiliwe huru

Wanawake wameandamana katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja wakitaka serikali imuachilie huru kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini humo Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake.

Wanawake hao ambao ni wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria INM wameandamana kwa amani nje ya Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu mjini Abuja wakitaka serikali imuachilie huru haraka na bila masharti Sheikh Ibrahim Zakzaki ambaye pia ni kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Nigeria.

Katika maandamano hayo ya hivi karibuni, wanawake hao ambao walikuwa wamebeba mabango ya kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru wameikosoa serikali kwa kuendelea kumshikilia mwanazuoni huyo wa Kiislamu pamoja na kuwa mahakama ya nchi hiyo imeamuru aachiliwe huru.

Itakumbukwa kuwa Sheikh Ibrahim Zakzaky akiwa na mke wake walitekwa nyara na Jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka 2015 wakati askari walipovamia kituo chake cha kidini huko katika mji wa Zaria jimboni Kaduna. Tokea wakati huo Sheikh Zakzaky na mkewe wamekuwa wakizuiliwa katika mojawapo ya vituo vya kijeshi vya nchi hiyo bila kufunguliwa mashktaka.

Wanawake wakiandamana kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru

Uvamizi huo ulijiri baada ya Jeshi la Nigeria kudai kuwa wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria walikuwa na njama ya kutaka kumuua mkuu wa jeshi hilo, madai ambayo yalikanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo.

Inakadiriwa kuwa Waislamu 1000 wasio na hatia waliuawa katika tukio hilo huku Sheikh Zakzaky, ambaye hali yake ya kiafya si nzuri, akiendelea kushikiliwa korokoroni pasina kufunguliwa mashtak

Tags