UN yawawekea vikwazo jenerali wa jeshi Congo DR, makamanda wa waasi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i39865-un_yawawekea_vikwazo_jenerali_wa_jeshi_congo_dr_makamanda_wa_waasi
Kamati ya Vikwazo ya Umoja wa Mataifa imeyaweka majina manne ya makamanda wengine wa kijeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika orodha yake nyeusi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 03, 2018 12:04 UTC
  • UN yawawekea vikwazo jenerali wa jeshi Congo DR, makamanda wa waasi

Kamati ya Vikwazo ya Umoja wa Mataifa imeyaweka majina manne ya makamanda wengine wa kijeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika orodha yake nyeusi.

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema kuwa, makamanda hao wanatambuliwa kuwa ni hatari sana kwa mujibu wa kifungu nambari 7 cha azimio nambari 2293 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. 

Jina la Jenerali Muhindo Akili Mundos wa jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pia linaonekana katika orodha hiyo nyeusi ya UN. Majina mengine matatu ni ya makamanda wa makundi ya waasi na makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha.

Waasi wanaobeba silaha Congo DR

Azimio nambari 2293 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipasishwa mwaka 2017. Mbali na kuweka vikwazo vya silaha na fedha, azimio hilo pia limeainisha vikwazo vya kusafiri kwa wale wote wanaotambuliwa kuwa wanakwaza mchakato wa kurejesha amani katika Jamhuri ya Kidemokraia ya Congo.