Kundi la kigaidi lenye uhusiano na Daesh laangamizwa Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i4942-kundi_la_kigaidi_lenye_uhusiano_na_daesh_laangamizwa_tunisia
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia imesema kuwa imelikamata kundi moja la kigaidi katika mkoa wa Bizerte kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 12, 2016 23:48 UTC
  • Kundi la kigaidi lenye uhusiano na Daesh laangamizwa Tunisia

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia imesema kuwa imelikamata kundi moja la kigaidi katika mkoa wa Bizerte kaskazini mwa nchi hiyo.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia imetangaza kuwa vikosi vya usalama vya nchi hiyo vimefanikiwa kuwatiwa mbaroni washukiwa watano kwa kuwa na uhusiano na magaidi huko katika eneo la Ras al Jebel katika mkoa wa Bizerte.

Baada ya kutiwa mbaroni, watu hao wamekiri kutangaza utiifu wao kwa kundi la kigaidi la Daesh an magaidi wengine wa Kitunisia ambao sasa wamekimbilia huko Syria.

Washukiwa hao watano wenye uhusiano na Daesh walitiwa mbaroni, baada ya mmojawao kusambaza katika mtandao wa kijamii wa facebook picha za maeneo mbalimbali ya magaidi.

Vikosi vya usalama vya Tunisia pia vimekamata pia simu ya mkononi kutoka kwa magaidi hao waliotiwa mbaroni na baada ya kuichunguza wamekuta picha ya mke wa gaidi mmoja kati ya hao waliotiwa nguvuni akiwa ameshika bendera ya kundi la kigaidi la Ansarul Sharia. Mume wa mwanamke huyo amekiri kuwa ameshiriki katika shughuli na vikao mbalimbali vya kundi la kigaidi la Daesh.