Ongwen kukata rufaa baada ya kuhukumiwa mahakama ya ICC
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i66890-ongwen_kukata_rufaa_baada_ya_kuhukumiwa_mahakama_ya_icc
Kamanda wa zamani wa waasi wa kundi la Lord’s Resistance Army, Dominic Dominic Ongwen amesema atakata rufaa dhidi ya uamuzi wa Februari 4 wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), ambayo ilimpata na hatia ya kutenda uhalifu 61 wa kivita jinai dhidi ya ubinadamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 15, 2021 09:41 UTC
  • Dominic Ongwen
    Dominic Ongwen

Kamanda wa zamani wa waasi wa kundi la Lord’s Resistance Army, Dominic Dominic Ongwen amesema atakata rufaa dhidi ya uamuzi wa Februari 4 wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), ambayo ilimpata na hatia ya kutenda uhalifu 61 wa kivita jinai dhidi ya ubinadamu.

Kiongozi wa timu ya mawakili wa Ongwen, Krispus Ayena Odongo amesema watakata rufaa kwa sababu uamuzi uliotolewa ni mbaya na kuna sababu kadhaa za kupinga hukumu iliyotolewa dhidi ya mteja wake ambayo iwapo itapasishwa yumkini akahukumiwa kifungo cha hadi miaka 30 jela.

Bw Odongo pia anasema kuwa Ongwen ni nhanga na alitekwa nyara mnamo 1988 na kulazimishwa kuingia katika safu za kundi la LRA akiwa mtoto wa miaka tisa. Hata hivyo, Mwendesha Mashtaka wa ICC Fatou Bensouda amesema kuwa uhalifu uliomtia hatiani kamanda huyo wa zamani wa kundi la LRA ni ule ulioufanya akiwa mtu mzima kati ya 2002 na 2005.

Dominic Ongwen alikabiliwa na mashitaka ya mauwaji, mateso, ubakaji na watu kugeuzwa watumwa.

Dominic Ongwen

Ongwen na kundi lake la waasi la Lord's Resistance Army anatuhumiwa kuhusika na mauwaji ya watu zaidi ya laki moja tangu mwaka 1987 na kuwateka nyara maelfu ya watoto.

Kesi hii ni muhimu kwa ajili ya kuwatendea haki raia walioathiriwa na jinai za kundi hilo la waasi wa Kikristo ambao waliua maelfu ya raia na kulazimisha wengine karibu milioni mbili kuwa wakimbizi.