Wanajeshi wa Mauritania waanza kulinda amani CAR katika kikosi cha UN
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i8020-wanajeshi_wa_mauritania_waanza_kulinda_amani_car_katika_kikosi_cha_un
Wanajeshi wa Mauritania wameanza kuhudumu katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 29, 2016 02:22 UTC
  • Wanajeshi wa Mauritania waanza kulinda amani CAR katika kikosi cha UN

Wanajeshi wa Mauritania wameanza kuhudumu katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Zaidi ya wanajeshi 740 wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa wamepangiwa kazi ya kulinda amani katika mikoa ya Ouaka na Basse-Kotto katikati mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, mikoa ambayo iliathiriwa sana na mapigano ya kikaumu. Sidi el Vereireck, kamanda wa kikosi hicho cha Mauritania amesema kuwa, wanajeshi wao wana zana zao za kijeshi na wamepata mafunzo mazuri ya ya kijeshi. Amesema, wametumwa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kuimarisha usalama. Kamanda wa wanajeshi wa kulinda amani wa Mauritania waliotumwa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ameongeza kuwa wametimiza vigezo vyote vilivyotakiwa na Umoja wa Mataifa.

Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia kwenye mapigano ya kikaumu tangu mwaka juzi. Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na wale wa Ufaransa walitumwa nchini humo tangu mwaka 2013 kwa madai ya kurejesha amani, hata hivyo hadi kufikia sasa usalama wa nchi hiyo ni wa kulegalega.