Jan 20, 2017 08:20 UTC
  • Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Jumuiya ya Wanachuo Ulaya

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe kwa jumuiya za Kiislamu za wanafunzi wa vyuo vikuu barani Ulaya na kusema: "Ni jukumu la kila mtu kupeperusha bendera ya Uislamu halisi katika vita visivyo na usawa vya makabiliano na mrengo wa kufru na uistikbari."

Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wake huo uliotolewa Ijumaa hii, amesema: "Ni matarajio yangu kuwa mbali na kuwa mtajijenga kielimu, kidini na kiakhlaqi, muwe pia ni wenye taathira katika mazingira yenu na muongoze watu zaidi wafuate njia ya Mwenyezi Mungu kwa maneno na vitendo vyenu vyema."

Ayatullah Khamenei ameashiria kuwa, 'ujana na uanachuo' ni nukta zenye nguvu ambazo humsaidia mwanadamu kufikia malengo yake ya juu' na kuongeza kuwa, 'mbali na kuwa muna sifa hizo mbili, pia mna sifa nyingine yenye taathira nayo ni kupitia jumuiya za Kiislamu.'

Kiongozi Muadhamu Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, kila moja anapaswa kunufaika na baraka za chemchemu ya maarifa sahihi ya Kiislamu na kuwa katika njia nyofu ya Mwenyezi Mungu.

Tags