Rais Rouhani ampongeza Rais Museveni kwa kuchaguliwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i2959-rais_rouhani_ampongeza_rais_museveni_kwa_kuchaguliwa
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amempongeza Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa kuchaguliwa tena hivi karibuni kuiongoza nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 13, 2016 03:46 UTC
  • Rais Rouhani ampongeza Rais Museveni kwa kuchaguliwa

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amempongeza Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa kuchaguliwa tena hivi karibuni kuiongoza nchi hiyo.

Katika ujumbe wake huo, Rais Rouhani amemtumia salamu za kheri na fanaka Museveni kufuatia kuchagiliwa tena.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ana matumaini kuwa, uhusiano wa Iran na Uganda utazidi kuimarika katika siku za usoni.

Tume ya Uchaguzi ya Uganda mwezi uliopita ilimtangaza Yoweri Museveni kuwa Rais Mpya wa nchi hiyo baada ya kushinda zaidi ya asilimia 60 ya kura na hivyo kumshinda mpinzani wake mkuu Dakta Kiiza Besigye katika uchaguzi wa Februari 18.

Museveni ambaye tangu miaka 30 iliyopita hadi sasa anatawala Uganda, ni kati ya Marais wa Afrika ambao wamezifanyia marekebisho katiba za nchi zao kwa kufuta kipengee kinachohusiana na ukomo wa mihula miwili ya kuwepo madarakani rais wa nchi; na hivyo kujiandalia njia ya kusalia madarakani.

Rais Museveni amesisitiza mara kwa mara kuwa demokrasia ya Afrika isilinganishwe na ya nchi za Magharibi.