Zarif: Wairani wote ni "Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu"
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i35659-zarif_wairani_wote_ni_walinzi_wa_mapinduzi_ya_kiislamu
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu yay Iran amesema katika radiamali yake kwa matamshi ya chuki na kiuadui ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwamba hii leo Wairani wote, wake kwa waume na vijana kwa wazee ni "Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu".
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 14, 2017 12:45 UTC
  • Zarif: Wairani wote ni

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu yay Iran amesema katika radiamali yake kwa matamshi ya chuki na kiuadui ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwamba hii leo Wairani wote, wake kwa waume na vijana kwa wazee ni "Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu".

Dakta Muhammad Javad Zarif ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba: Kwa nguvu zao zote, Wairani wote wako bega kwa bega na watu wanaoihami Iran na eneo la Mashariki ya Kati na uvamizi na mauaji.

Jana Ijumaa Rais Donald Trump wa Marekani  alitoa matamshi ya kijinga na akakariri tuhuma zisizo na maana za huko nyuma  dhidi ya taifa la Iran; na kwa hatua yake ya kutothibitisha na kutoidhinisha kufungamana Iran na makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA, kwa mara nyyingine tena alidai kwamba, eti Tehran inaunga mkono ugaidi na akaliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH katika orodha ya vikwazo vipya.

Rais Donald Trump wa Marekani

Hii ni katika hali ambayo, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH limekuwa likitoa ushauri katika vita dhidi ya kundi la kigaidi na kitakfiri huko Syria na Iraq kutokana na maombi rasmi ya nchi hizo kwa Iran.

SEPAH imekuwa na nafasi muhimu katika vita dhidi ya ugaidi unaoungwa mkono na Marekani.