Iran yaijibu Bahrain inayodai Quds si suala muhimu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i37917-iran_yaijibu_bahrain_inayodai_quds_si_suala_muhimu
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu hatua ya hivi karibuni ya waziri wa mambo ya nje wa Bahrain aliyeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa eti kadhia ya Quds na Palestina si muhimu bali ni suala la pembeni tu.
(last modified 2026-01-14T11:42:18+00:00 )
Dec 22, 2017 04:24 UTC
  • Iran yaijibu Bahrain inayodai Quds si suala muhimu

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu hatua ya hivi karibuni ya waziri wa mambo ya nje wa Bahrain aliyeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa eti kadhia ya Quds na Palestina si muhimu bali ni suala la pembeni tu.

Akijibu hatua hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain, Khalid bin Ahmed Aal Khalifa, Bahram Qassemi amesema, licha ya kuweko njama na hila za kila namna za kuzusha migogoro bandia, lakini kadhia ya Palestina itaendelea kuwa suala muhimu zaidi kwa ulimwengu wa Kiislamu hadi zitakapokombolewa ardhi zote za taifa hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain, Khalid bin Ahmed Al Khalifa

 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain amedai katika ukurasa wake wa Twitter kwamba hakuna haja ya kujiingiza katika mgogoro na Marekani katika suala la Palestina. Itakumbukwa kuwa ukoo wa Aal Khalifa sawa na Aal Saud ni vibaraka wakuu wa Marekani.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, hakuna mtu wala nchi yoyote inayoweza kuitoa kadhia ya Palestina katika moyo wa umma wa Kiislamu kwani Palestina ni sehemu muhimu sana ya ulimwengu wa Kiislamu.

Suala la Palestina si muhimu tu kwa ulimwengu wa Kiislamu, bali ni kadhia muhimu kwa dunia nzima. Jana Alkhamisi, wanachama wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa walipasisha kwa kura mutlaki muswada wa kuiunga mkono Quds na kudharau vitisho vyote vilivyotolewa na Marekani kura hiyo.