'Iran haishughulishwi na makelele ya Marekani; itaimarisha majaribio ya makombora yake'
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i50334-'iran_haishughulishwi_na_makelele_ya_marekani_itaimarisha_majaribio_ya_makombora_yake'
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, SEPAH, limeapa kuwa litaendelea na majaribio na utafiti wake wa makombora kwa kasi zaidi ya huko nyuma na litapuuza mashinikizo na vikwazo vya Marekani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 22, 2018 03:03 UTC
  • 'Iran haishughulishwi na makelele ya Marekani; itaimarisha majaribio ya makombora yake'

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, SEPAH, limeapa kuwa litaendelea na majaribio na utafiti wake wa makombora kwa kasi zaidi ya huko nyuma na litapuuza mashinikizo na vikwazo vya Marekani.

Hayo yamedokezwa na Naibu Kamanda wa SEPAH anayeshughulikia uratibu Brigedia Jenerali Ali Fadavi alisema hayo jana Ijumaa katika mahojiano na shirika la habari la IRNi. Ameongeza kuwa, kufanya utafiti na majaribio ya makombora na jukumu la kudumu la Jeshi la Wainzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Brigedia Jenerali Fadavi amesema utafiti na majaribio ya makombora ni sawa na kuvuta pumzi na kwa Iran na amehoji, "Je unaweza kumzuia mtu kuvuta pumzi?"

Ameashiria mashinikizo na vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kusema, hiyo ni fursa ya kuiwezesha Iran kujitegemea. Amesema kadiri vikwazo vinavyokuwa vikali ndipo uwezo wa Iran wa kujitegemea katika kijihami unavyozidi kuongezeka.

Naibu Kamanda wa IRGC anayeshughulikia uratibu Brigedia Jenerali Ali Fadavi

Wiki iliyopita, Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh, Kamanda wa Kitengo cha Angani cha SEPAH alisema kuwa: "Kila mwaka Iran hufanya majaribio 40 hadi 50 ya makombora.

Jumamosi iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif alisisitiza kwa mara nyingine kuwa, Tehran kamwe haitafanya mazungumzo kuhusu makombora yake ya kujihami.

Zarif aliyasema hayo  katika mazungumzo na mwandishi wa Televisheni ya Al Jazeera pembizoni mwa  "Mkutano wa Doha" uliofanyika katika mji mkuu wa Qatar na alikanusha madai ya wakuu wa Marekani akiwemo rais wa nchi hiyo, Donald Trump, kuwa eti Iran inakiuka azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Zarif alisema ni Marekani ndiyo ambayo imekiuka azimio hilo na hivyo haina ustahiki wa kuituhumu Iran.