Apr 30, 2016 04:08 UTC
  • Iran: Dunia iungane katika vita dhidi ya ugaidi

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeonya kuhusu kuenea ugaidi na misimamo mikali duniani na kusema jamii ya kimataifa inapasa kushirikiana kukabiliana na uovu huo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran Morteza Sarmadi alipozungumza na waandishi habari baada ya Mkutano wa Tano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Kongamano la Maingiliano na Hatua za Kuaminiana ASIA (CICA) mjini Beijing Uchina, Ijumaa.

Ameongeza kuwa kuwa dunia inashuhudia kuongezeka ugaidi, taasubi za kimadhehebu na makudni wa wakufurishaji na hivyo kupelekea hali kuwa ngumu katika nchi nyingi hasa Mashariki ya Kati.

Sarmadi ametoa wito kwa nchi za Asia kushirikiana kwani kukabiliana na ugaidi ili eneo hilo lishuhudie amani na usalama. Aidha amebainisha azma ya Iran ya kuimarisha ushirikiano wa nchi za CICA.

Tags