Radiamali ya Iran kufuatia kutangazwa matokeo ya kura ya maoni ya Uingereza
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i9913-radiamali_ya_iran_kufuatia_kutangazwa_matokeo_ya_kura_ya_maoni_ya_uingereza
Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoao taarifa kuhusu matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika nchini Uingereza kuhusu kujiondoa nchi hiyo katika Umoja wa Ulaya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 25, 2016 01:57 UTC
  • Radiamali ya Iran kufuatia kutangazwa matokeo ya kura ya maoni ya Uingereza

Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoao taarifa kuhusu matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika nchini Uingereza kuhusu kujiondoa nchi hiyo katika Umoja wa Ulaya.

Hussein Jaberi Ansari Msemaji wa Zamani wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ambaye hivi sasa ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya nchi za Kiarabu na Afrika ametoa taarifa katika mtandao wake wa kijamii akisema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa ni nchi ya mfumo wa kidemokrasia inaheshimu uamuzi huo wa kura za wananchi wa Uingereza wa kujiondoa katika Umoja wa Ulaya; na kwamba Iran inaihesabu hatua hiyo kuwa takwa la waliowengi huko Uingereza kwa ajili ya kuweka sawa uhusiano wao wa nje.

Taarifa ya Hussein Jaberi Ansari imeongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku zote inataka kuimarisha uhusiano kati yake na nchi za Ulaya kwa msingi wa kuheshimiana pande mbili na nchi yoyote kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine. Amesema kujiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya hakutabadilisha mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu nchi hiyo.