Apr 04, 2024 06:52 UTC
  • Hassan Nasrullah: Kimbunga cha al-Aqsa kimemsukuma adui Mzayuni kwenye ukingo wa shimo la mauti

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu ni tofauti na miaka iliyopita, na kwamba operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa imemweka adui Mzayuni kwenye ukingo wa shimo la mauti.

Akizungumza kwa njia ya mawasiliano ya video hapo jana Jumatano mbele ya viongozi na shakhsia wa mhimili wa muqawama katika kukaribia maadhimisho ya Siku ya Kiamataifa ya Quds kesho Ijumaa, Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya nchini Lebanon, amesema: Kile kinachoendelea Palestina na eneo zima la Asia Magharibi ni Kimbunga cha Waliohuru na tunatumai kuwa kitaenea na kupata nguvu zaidi."

Nasrallah ameongeza kuwa: "Adui hajali maazimio ya Baraza la Usalama, matakwa ya nchi, maoni ya umma wala sheria za kimataifa."

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema: 'Ni lazima tufanye kazi kwa bidii ili tushinde vita hivi na kumshinda adui Mzayuni na waungaji mkono wake wote, na hili lazima liwe lengo letu kuu.'

Seyyed Hassan Nasrallah amesema kuwa, vita vya siku 33 viliushinda mpango wa Mashariki ya Kati Mpya na mpango wa Israel Kubwa na kusisitiza kwamba: "Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa imeuweka utawala wa Kizayuni kwenye ukingo wa kuporomoka na kuangamia, na dalili za suala hili zitadhihirika zaidi katika siku zijazo."

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema: "Ni lazima tusisitize kwamba kuwa imara na ushindi wa mwisho ni jambo la hakika, na hili linahusiana na Gaza na pande zote zinazounga mkono na kushiriki katika vita hivi."

Hassan Nasrallah amefafanua zaidi kwa kusema: "Ni lazima tufanye juhudi zote kwa ajili ya kufanikisha Kimbunga cha al-Aqsa kufikia malengo yake na hili ni jukumu letu sote."

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon aidha amesema: "Wajibu wetu katika Siku ya Kimataifa ya Quds ni kubainisha matokeo ya kistratijia ya operesheni ya Kimbgunga cha al-Aqsa na hasa kushindwa kistratijia kwa mipango ya Wamarekani na Wazayuni katika eneo. Majukwaa na vyombo vyote vya habari vinavyounga mkono muqawama ni kuakisi mafanikio ya operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa, vinginevyo, adui atapotosha ukweli na kufanya mafanikio ya kihistoria ya muqawama yaonekane kuwa yamefeli."

Tags