Apr 18, 2024 04:24 UTC
  • Watoto elfu 19 wa Kipalestina wamekuwa mayatima kutokana na jinai za Israel Ukanda wa Gaza

Watoto 19,000 wa Kipalestina wamekuwa mayatima kufuatia jinai za kinyama za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr, Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa wanawake wa Kipalestina zaidi ya elfu kumi wameuawa shahidi katika vita na mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.  

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa: Makumi ya maelfu ya wanawake pia wamelazimika kuhama makazi yao na sasa wamekuwa wakimbizi kutokana na  mashambulizi ya mabomu ya jeshi la Kizayuni tangu kuanza kwa vita na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza.  

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watoto 19,000 wa Kipalestina wamekuwa yatima kufuatia kuuliwa shahidi akina mama elfu sita katika mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Gaza.  

Wanawake elfu sita wa Ukanda wa Gaza wameuliwa shahidi na utawala wa Kizayuni 

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeongeza kuwa: Zaidi ya wanawake na wasichana milioni moja katika Ukanda wa Gaza hawana chakula na maji salama; na wanaishi katika hali mbaya sana ya kibinadamu. 

 

Tags