Wasiwasi wa kimataifa kuhusu mgogoro wa kibinadamu Ukanda wa Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103690-wasiwasi_wa_kimataifa_kuhusu_mgogoro_wa_kibinadamu_ukanda_wa_ghaza
Shambulio la utawala wa Kizayuni katika hospitali huko katika Ukanda wa Ghaza limelaaniwa na pande mbalimbali kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 19, 2023 23:07 UTC
  • Wasiwasi wa kimataifa kuhusu mgogoro wa kibinadamu Ukanda wa Ghaza

Shambulio la utawala wa Kizayuni katika hospitali huko katika Ukanda wa Ghaza limelaaniwa na pande mbalimbali kimataifa.

Katika jinai ya karibuni dhidi ya binadamu, maghasibu wa Kizayuni Jumanne usiku wiki hii waliishambulia hospitali ya Al Maamadani huko Ukanda wa Ghaza na kuwaua shahidi Wapalestina zaidi ya 500.  

Shambulio la Wazayuni dhidi ya hospitali ya Al Maamadani huko Ghaza 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan ametoa radiamali yake kwa shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya hospitali ya Ghaza kwa kusema: Mawaziri wa Mambo ya Nje wa kundi la G-7 wameeleza kutiwa wasiwasi na hali ya mambo katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kusisitiza kuboreshwa hali ya kibinadamu ya Ukanda wa Ghaza. Yoko Kamikawa amesema  Kundi la G-7  limeahidi kushirikiana ili kuhitimisha vita huko Ghaza. 

Hata kama G-7 inatoa indhari kuhusu mgogoro wa kibinadamu huko Ghaza lakini si siri kwa walimwengu kwamba chanzo kikuu cha hali ya mgogoro huo na mauaji ya raia wa Palestina ni baadhi ya nchi wanachama wa kundi la G-7 khususan Marekani, ambazo zinaendelea kuzuia kusitishwa mauaji ya watu wa Ghaza kwa hatua yao ya kukataa kufuatialia juhudi za usitishaji vita katika ukanda huo. 

Farhad Amin mchambuzi wa masuala ya kimataifa anazungumzia hil kwa kusema: Nchi za Magharibi wanachama wa G-7 ni chanzo kikuu cha mgogoro unaowakabili Wapalestina; na uungaji mkono wa nchi hizo kwa Wazayuni unazidi kuwapa kiburi maghasibu hao cha kuendeleza mauaji ya kiholela dhidi ya Wapalestina huko Ghaza. Kwa msingi huo, iwapo matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan kwamba kundi la G-7 linatiwa wasiwasi na mgogoro wa kibinadamu huko Ghaza ni ya kweli; swali kuu linalojitokeza hapa ni kuwa, je, kwa nini nchi hizo hazichukui hatua mara moja ili kusitisha mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya Wapalestina?

Kwa msingi huo, Anwar Haq Kakar Waziri Mkuu wa muda wa Pakistan ametaja mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya hopistali na kambi za wakimbizi kuwa ni hatua isiyo ya kibinadamu na isiyoweza kutetewa kivyovyote ambayo ni kinyume na sheria za kimataifa kuhusu masuala ya kibinadamu zinazobainisha juu ya  kulindwa hospitali na wafanyakazi wa sekta ya afya na tiba. Kakar ameashiria mazungumzo aliyofanya na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko China na kuongeza kuwa: Tunataka kuhitimisha mashambulizi haya ya kiholela na tunatoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua haraka iwezekanavyo kusitisha machafuko ya utawala wa Israel na wachokozi kuwajibishwa. 

Anwar Haq Kakar, Waziri Mkuu wa muda wa Pakistan 

Hii ni katika hali ambayo watendaji jinai wa Kizayuni wanafanya kila wawezalo kuwaua raia wa Ghaza ili eti kufidia kichapo na kushindwa kwao pakubwa katika oparesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa. Hata hivyo hujuma na mashambulizi dhidi ya maeneo ya umma yamewakasirisha na kuwaghadhibisha pakubwa walimwengu mkabala wa utawala wa Kizayuni  unaotenda jinai na waungaji mkono wake. 

Molavi Mofleh mchambuzi wa masuala ya Mashariki ya Kati anasema: "Utawala wa kibaguzi wa Kizayuni unafahamu vyema unaishi kwenye nyumba dhaifu na ya vioo; na karibuni nyumba hii itaharibiwa kikamilifu na kukabidhiwa kwa wamiliki wake wa asili." Mauaji ya raia yanayofanywa na Wazayuni ni katika kulipiza kisasi tu cha kushindwa pakubwa utawala huo mbele ya Kimbunga cha Al Aqsa; ambapo hata hivyo utawala huo kwa njia hii hautaweza kufanikisha malengo yake." 

Al Kul haal,  Wizara ya Mambo ya Nje ya  Tajikistan pia imeungana na nchi nyingine duniani na kulaani vikali shambulio la Wazayuni dhidi ya hospitali ya Al Maamadani huko Ghaza, jinai ambayo imelalamikiwa pakubwa na aghalabu ya nchi duniani. Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa sheria za kimataifa, taasisi za kiraia na hasa hospitali kwa hali yoyote ile hazipasi kushambuliwa wala kuhujumiwa bali zinapasa kuwa maeneo salama kwa ajili ya kutoa huduma kwa waanchi katika kila hali. Kwa hiyo, mashambulizi ya Wazayuni katika maeneo kama hayo ni doa jeusi kwenye vipaji vya nyuso zao na za waungaji mkono wao, khususan Marekani.

Jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Kipalestina wa Ukanda wa Ghaza 

Wakati huo huo kunyamaza kimya nchi za Magharibi na wale wanaojinadi kutetea haki za binadamu duniani mbele ya jinai za Wazayuni huko Ghaza kumewathibitishia walimwengu kwamba Marekani inaunga mkono ugaidi na mauaji ya raia wasio na hatia, na inazidi kuchochea jinai za utawala wa Kizayuni kwa uungaji mkono wake wa pande zote kwa utawala huo ghasibu.