Kuangamizwa askari wengine 11 wa Kizayuni huko Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i105942-kuangamizwa_askari_wengine_11_wa_kizayuni_huko_gaza
Wanajeshi wengine 11 wa Kizayuni wameangamizwa katika vita vya wanamapambano wa Kipalestina, Hamasa katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2024-05-29T07:24:47+00:00 )
Dec 13, 2023 04:21 UTC
  • Kuangamizwa askari wengine 11 wa Kizayuni huko Gaza

Wanajeshi wengine 11 wa Kizayuni wameangamizwa katika vita vya wanamapambano wa Kipalestina, Hamasa katika Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, vikosi vya al-Qassam  tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) vimelenga magari saba ya kijeshi ya Kizayuni kwa roketi na mabomu ya kulipua vifaru katika kitongoji cha Al-Shajaiyeh huko Gaza na kuwaangamiza askari wote waliokuwemo.

Leo, na katika siku ya 67 ya vita huko Gaza, Redio ya Jeshi la Israel imetangaza idadi ya wanajeshi wake waliojeruhiwa tangu kuanza mapigano ya nchi kavu kuwa ni askari 111.

Redio hiyo pia imetangaza kuwa wanajeshi wake 20 wameangamizwa katika mashambulizi ya vikosi vyake huko Gaza na kuwa 13 kati yao walilengwa na wapiganaji wa Palestina.

Wizara ya Afya ya Gaza imetangaza kuwa Wazayuni wameshambulia hospitali, wafanyakazi wa afya na kuwa takriban watu elfu 8 waliojeruhiwa wanahitaji kufanyiwa upasuaji wa haraka.

Msimamizi wa wizara hiyo ameeleza kuwa takriban wagonjwa 600, wakiwemo majeruhi 413, wametumwa katika kivuko cha Rafah kwa ajili ya kupata matibabu nje ya Ukanda wa Gaza.

Wizara hiyo imeongeza kuwa, tangu kuanza uvamizi wa utawala wa Kizayuni tarehe 7 Oktoba, watu 18,412 wameuawa shahidi na zaidi ya 50,000 wamejeruhiwa.