Idadi ya mashahidi Gaza yakaribia watu 20,000
Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza ongezeko la idadi ya mashahidi na majeruhi katika mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kigaidi wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza katika takwimu mpya kwamba, idadi ya mashahidi wa Kipalestina tangu kuanza hujuma ya utawala wa Kizayuni huko Gaza (Oktoba 7) imefikia zaidi ya 19,888.
Ikiashiria kuwa Wapalestina 54,450 walijeruhiwa, shirika hili la Wapalestina limesema kuwqa, asilimia 70 ya mashahidi huko Gaza ni wanawake na watoto, na wengi wamepotea.
Wizara ya Afya ya Palestina imeongeza kuwa, zaidi ya wafanyakazi 300 wa sekta ya afya, vikosi 35 vya ulinzi wa raia na wafanyakazi 135 wa Shirika la Misaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) wameuawa shahidi katika hujuma inayoendelea ya utawala ghasibu wa Israel.
Kulingana na ripoti hiyo, mafuta huko Gaza yanakaribia kumalizika na suala hili litakuwa na matokeo mabaya ya kiafya kwa watoto, na kwa sasa kesi 360,000 zimeripotiwa za magonjwa ya kuambukiza.
Kulingana na shirika hili la Wapalestina, kati ya hospitali 36 za Ukanda wa Gaza, ni hospitali 11 tu ndizo zinazofanya kazi kwa kutoa huduma ndogo ndogo tena huduma chache sana.
Wakati huo huo, wanamapambano wa Brigedi za Izuddin al Qassam, Tawi la Kijeshi la HAMAS na makundi mengine ya muqawama wa Palestina yanaendelea na mapambano yao makali na kutoa vipigo kwa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni waliovamia Ukanda wa Gaza.
Katikka upande mwingine, duru za muqawama wa Palestina zimesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unachuja mno habari kuhusu vipigo unavyopata huko Ghaza na pamoja na hayo idadi ya hasara ambayo utawala huo wenyewe unakiri kuzipata kila siku, ni kubwa.