WHO yaonya kuhusu kutokea maafa ya kibinadamu Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i106780-who_yaonya_kuhusu_kutokea_maafa_ya_kibinadamu_gaza
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amelaani shambulio la bomu katika kituo cha Hilali Nyekundu cha Palestina katika Ukanda wa Gaza, na kuitaja hatua hiyo kwamba, iikko kkinyume na dhamiri na takkwa la kulinda vituo vya matibabu katika ukanda huo.
(last modified 2024-01-03T23:40:39+00:00 )
Jan 03, 2024 23:40 UTC
  • WHO yaonya kuhusu kutokea maafa ya kibinadamu Gaza

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amelaani shambulio la bomu katika kituo cha Hilali Nyekundu cha Palestina katika Ukanda wa Gaza, na kuitaja hatua hiyo kwamba, iikko kkinyume na dhamiri na takkwa la kulinda vituo vya matibabu katika ukanda huo.

Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani sambamba na kulaani mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya kituo cha Hilali Nyekundu huko Khan Yunis, ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba wengi wa watu 14,000 waliopata hifadhi katika hospitali hiyo wamelazimika kuondoka katika eneo hili huku waliobakia wakiwa na wasiwasi mkubwa kuhusiana na usalama wao.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limeonya kwamba asilimia 40 ya wakazi milioni 2.3 wa Gaza wanakabiliwa na hatari ya njaa, wakati huu ambapo utawala wa Kizayuni wa Israel unaendeleza vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika eneo hilo linalozingirwa.

Ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa, kuhusu hali mbaya ya Ukanda wa Gaza kuwa, Israel imebomoa asilimia 70 ya majengo na makazi ya Gaza; na hadi kufikia katikati ya mwezi uliopita wa Disemba makombora na mabomu zaidi ya elfu 29 yalikuwa yameangushwa katika eneo hilo.

 

Uharibifu mkubwa wa Gaza kutokana na mashambulizi ya kinyama ya jeshi katili la Kizayuni umekuwa na madhara makubwa kwa Wapalestina wanaoishi katika ukanda huo.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, shule 352 ambazo ni sawa na asilimia 70 ya shule za Gaza zimeharibiwa vibaya katika mashambulizi ya jeshi vamizi la Israel.