Wanajeshii watano wa Israel waangamizwa na muqawama Khan Yunis
Wanajeshi watano wa utawala vamizi wa Israel wameuawa na wengine kadhaa kuujeruhiwa katika mapigano baina yao na wanamuqawama wa Palestiona katika mji wa Khan Yunis huko Palestina.
Shirika la Habari la Mehr linaripoti kuwa, mujahidina wa Brigedi za Izzuddin Qassam tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS wamekabiliana na wanajeshi wa Israel mashariki mwa Khan Yunis kusini mwa Ukanda wa Gaza na kuwaangamiza watano kati yao.
Aidha wanajeshi kadhaa wa Israel wamejeruhiwa katika mapigano hayo.
Kuuawa kwa wanajeshi hao watano wa jeshi la utawala haramu wa Israel huko Khan Yunis kunaifanya idadi ya askari Israel walioangamizwa hadi sasa tangu ilipototekelezwa operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa kufikia 527.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa, idadi ya askari wa Israel waliouawa ni zaidi ya hiyo hasa kutokana na mamlaka husika kutotoa takwimu sahihi.
Utawala dhalimu wa Israel ambao umeshindwa kwenye medani za mapambano, umeamua kumalizia hamaki zake kwa kuua watoto wadogo, wanawake, vizee na raia wa kawaida huko Gaza.
Katika upande mwingine, imeelezwa kuwa, wakati mfumo wa afya ya akili wa Israel unakabiliwa na hatari ya kuporomoka, madaktari wa magonjwa ya akili wanaondoka kuelekea Uingereza kutafuta hali bora zaidi ya maisha.
Kugura huko kwa madaktari wa afya ya akili kunakuja wakati mahitaji ya huduma za afya ya akili huko Israel yanaongezeka kutokana na vita vya Gaza, na kwamba wiki iliyopita wakuu wa vituo vya afya ya akili walituma barua kwa Mdhibiti wa Serikali, Matanyahu Englman, wakionya kwamba "mfumo wa afya ya akili wa Israel unakaribia kusambaratika kabisa.”