Abdollahian: Iran iko tayari kushirikiana na Ulaya kwa kuzingatia maslahi ya pamoja
(last modified Sat, 11 May 2024 04:14:04 GMT )
May 11, 2024 04:14 UTC
  • Abdollahian: Iran iko tayari kushirikiana na Ulaya kwa kuzingatia maslahi ya pamoja

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran iko tayari kushirikiana na Ulaya kwa kuzingatia maslahi ya pande mbili.

Hussein Amir-Abdollahian amesema hayo katika ujumbe wake kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwa mnasaba wa Siku ya Ulaya, na kusisitiza kwamba, Iran iko tayari kuendelea kufanya kazi na kushirikiana na Ulaya kwa misingi ya heshima na kujenga, mazungumzo na ushirikiano katika mwelekeo wa maslahi ya pamoja na amani na usalama duniani.

Amir-Abdollahian ameongeza kuwa: Katika siku hii maalumu, wale wote ambao wamefanya kazi kwa ajili ya amani na ustawi wa Ulaya wanapaswa pia kufikiria kuhusu amani na usalama katika dunia nzima.

Aidha Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iranamesema, kinachotokea katika Ukanda wa Gaza ni mzigo mzito kwa dhamiri ya ubinadamu na mtihani mkubwa kwa uhalali wa maadili kama vile utu na haki za binadamu ambazo madola ya Ulaya yanapigia upatu jambo hilo na kudai kujitahidi katika hilo.

Mwishoni mwa ujumbe huo kawenye ukuurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Ulaya inapaswa kupaza sauti yake ya kutaka uadilifu katika kadhia ya Palestina.

Tags