Urusi yaitaka Uturuki kuacha kuwasaidia magaidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i4432-urusi_yaitaka_uturuki_kuacha_kuwasaidia_magaidi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameitaka Uturuki kuacha kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine na kuunga mkono ugaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 04, 2016 23:54 UTC
  • Urusi yaitaka Uturuki kuacha kuwasaidia magaidi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameitaka Uturuki kuacha kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine na kuunga mkono ugaidi.

Sergei Lavrov amesema ni muhimu kwa Uturuki kukomesha tabia ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine sawa iwe Syria au Iraq na kwamba kuna ushahidi wa kutosha unaothibitisha kwamba, Uturuki inaingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine ya kuunga mkono ugaidi.

Serikali ya Uturuki inalaumiwa kwa kuyaunga mkono na kuyasaidia makundi ya kigaidi yanayoajiri wapiganaji kutoka nje na kuingia Syria kupitia ardhi ya Uturuki kwa shabaha ya kuiondoa madarakani serikali halali ya Rais Bashar Assad.

Mapema mwezi huu balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa, Vitaly Churkin alisema kuwa, ushahidi unathibitisha kuwa Ankara inatuma silaha na zana za kijeshi kwa kundi la kigaidi la Daesh huko Syria kwa kutumia njia ya anga.

Russia pia imerusha hewani mkanda wa video unaoonesha jinsi serikali ya Uturuki inavyonunua mafuta kutoka kwa kundi la kigaidi la Daesh kwenye maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo huko Syria. Biashara hiyo ya mafuta inasimamiwa na mtoto wa kiume wa Rais wa Uturuki, Bilal Erdogan