Nasrullah: Makundi ya kigaidi nchini Syria yanasambaratika
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46453-nasrullah_makundi_ya_kigaidi_nchini_syria_yanasambaratika
Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema matukio yanayojiri katika eneo la Mashariki ya Kati yana manufaa kwa kambi ya muqawama na mapambano na kwamba makundi yanayobeba silaha huko Syria yamo katika hali ya kusambaratika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 29, 2018 23:40 UTC
  • Nasrullah: Makundi ya kigaidi nchini Syria yanasambaratika

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema matukio yanayojiri katika eneo la Mashariki ya Kati yana manufaa kwa kambi ya muqawama na mapambano na kwamba makundi yanayobeba silaha huko Syria yamo katika hali ya kusambaratika.

Sayyiid Hassan Nasrullah aliyasema hayo katika hotuba yake ya jana Ijumaa na kuongeza kuwa, japokuwa hali ya sasa Mashariki ya Kati ina manufaa kwa kambi ya mapambano lakini kuna watu wanaotumia matukio hayo vibaya na kuna udharura wa kukomeshwa jambo hilo.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ameashiria kushindwa kwa makundi ya kigaidi huko Syria na kusema kuwa, vita vya Syria ni vita vya eneo zima la Mashariki ya Kati na mustakbali wake na hii leo kunaonekana ishara za kusambaratika makundi ya kigaidi huko kusini mwa Syria. 

Vilevile ametoa wito kwa wakimbizi wa Syria kurejea nchini kwao kwa hiari na kwamba harakati ya Hizbullah iko tayari kutoa msaada kuhusu suala hilo. 

Makundi ya kigaidi ya Kiwahabi yanayoungwa mkono na Marekani, Israel, Saudia, Imarati nk 

Katibu Mkuu wa Hizbullah pia ameashiria mashambulizi ya anga yaliyofanywa dhidi ya makundi ya mapambano huko Iraq karibu na mpaka wa nchi hiyo na Syria na kusema: Mashambulizi hayo hayapasi kupita hivi hivi bila ya kujibiwa. 

Kuhusu hatua ya Marekani na kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, Sayyid Hassan Nasrullah amesema: Kujiondoa kwa Marekani katika makubaliano hayo, vitisho na vikwazo dhidi ya Iran ni sehemu ya mpango wa Marekani uliopewa jina la "Makubaliano ya Karne" ambayo lengo lake kuu ni kufuta kabisa kadhia ya Palestina.