Uungaji mkono wa Facebook kwa siasa za kigaidi za Israel
(last modified Tue, 27 Nov 2018 08:13:17 GMT )
Nov 27, 2018 08:13 UTC
  • Uungaji mkono wa Facebook kwa siasa za kigaidi za Israel

Mtandao wa kijami wa Facebook umepiga marufuku kusambazwa picha za kikosi maalumu cha ugaidi cha utawala wa Kizayuni katika oparesheni iliyofanywa hivi karibuni huko Ukanda wa Ghaza.

Jumapili usiku tarehe 11 mwezi huu wa Novemba kundi la makomando wa jeshi la utawala wa Kizayuni huku likitumia gari ya kiraia liliwasili katika eneo moja mashariki mwa mji wa Khan Yunis na kumuua kigaidi Noor Barakah mmoja wa makamanda wa brigedi ya shahidi Izzudin Qassam. Brigedi za Izzudin Qassam tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) hivi karibuni zilisambaza baadhi ya picha za waliotekeleza oparesheni ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni huko Khan Yunis na magari yaliyotumiwa katika oparesheni hiyo. Hatua hiyo ya Facebok iliyo dhidi ya vyombo vya habari  ambayo ni kinyume na misingi ya uhuru wa upashaji habari imechukuliwa katika hali ambao awali mwaka huu wa 2018 mtandao huo wa kijamii ulizuia pia kurasa za wanaharakati 100 wa Palestina na huko nyuma pia ilikuwa imezuia kurasa 200 za Wapalestina katika mtandao huo wa kijamii kwa tuhuma za kufanya uchochezi dhidi ya utawala wa Kizayuni. 

Makomando wa Israel waliokuwa wamejificha katika mpaka wa Ghaza kabla ya oparesheni ya Khan Yunis
 

Ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa Facebook ina mfungamano mkubwa na Israel na nyuma yake wakiwemo pia mamafia ambao kwa upande mmoja wana uhusiano na Wazayuni na kwa upande wa pili na viongozi wa Marekani. Waasisi na maafisa husika wa Facebook kwa kiasi kikubwa wamedhihirisha wazi malengo yao ya nyuma ya pazia ya kuratibu na kuasisi tovuti za aina hiyo. Mark Zuckerberg ndiye Mwasisi wa mtandao wa kijamii wa Facebook. Tovuti ya Kiyahudi au isiyo ya Kiyahudi kwa jina la (Jew or not Jew)  ambayo inatambulika kuwa sehemu ya kuainisha iwapo mtu ni Myahudi au si Myahudi  kwa mujibu wa uchunguzi wa kiushahidi na vigezo vya pande kadhaa imempatia pointi nyingi Mark Zuckerberg na hiyo inamaanisha kuwa yeye ana nafasi maalumu miongoni mwa Wazayuni. Zuckerberg amezaliwa katika familia ya Wayahudi wa Kimarekani. Aidha mwasisi huyo wa Facebook ameshika nafasi ya nne akitanguliwa na nafasi tatu baada ya Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel ambaye ametajwa kushika nafasi ya kwanza katika orodha iliyochapishwa na gazeti la Kizayuni la Jerusalem Post kuwa miongoni mwa Wayahudi 50 wenye nafasi athirifu zaidi. Miongoni mwa mameneja wengine wa Kizayuni wa Facebook pia tunaweza kumtaja Dustin Moskovitz rafiki Myahudi wa Zuckerberg ambaye amesaidia kuuendeleza mtandao huo wa kijamii na vile vile Marc Andreessen mmoja wa wawekezaji wa Facebook na mingoni mwa wawekezaji wa Shirika la Israel Fundamental Partners.

Marc Zuckerberg, Mwasisi wa Mtandao wa kijamii wa Facebook 
 

Kile ambacho zaidi ya yote kinatilia shaka madai ya uadilifu na kutoegemea upande wowote ya Facebook ni  utendaji wa mtandao huo wa kijamii ulivyo na mfungamano na siasa za Marekani na Israel. Mbali na ujasusi wa niaba wanaofanyiwa watumiaji wa Facebook; mtandao huo wa kijamii kwa picha ya kidhahiri hukabiliana na uanzishwaji wa aina yoyote wa makundi ya kijamii ambao unapingana na maslahi na siasa za Marekani na Uzayuni. Mifano ya wazi ya hatua hizo za Facebook tunaweza kushuhudia namna kurasa za mtandao huo wa kijamii zinazomilikiwa na wafuasi wa muqawama wa wananchi wa Palestina zinavyokabiliwa na vizuizi mbalimbali. Miongoni mwa hatua hizo tunaweza kuashiria kufutwa kwa ukurasa wa tangazo la wito wa Intifadha ya Tatu ya wananchi wa Palestina. Aidha duru mbalimbali za habari zinaarifu namna Israel inavyowafanyia ujasusi watumiaji wa Facebook na Twitter kwa uratibu wa waendeshaji wa mitandao hiyo. Kuhusiana na suala hilo, Mtandao wa Weak Leaks umefichua kwamba utawala wa Kizayuni  umeasisi huko Tel Aviv kituo cha kufuatilia na kuwadhibiti watumiaji wa mitandao ya kijamii kote duniani. Hii ni katika hali ambayo kitambo nyuma Facebook ilikiri kwamba watu milioni 87 wanaotumia mtandao huo duniani wako katika hatari ya kufichuliwa taarifa zao. Utendaji wa Facebook na msingi wa waendeshaji wa mtandao huo wa kijamii unaonyesha kuwa mtandao huo sawa kabisa na mingine ya nchi za Magharibi uko bega kwa bega kikamilifu na utawala wa Kizayuni katika kufanya ujasusi na kutekeleza ugaidi.