Dec 18, 2018 15:36 UTC
  • Zarif amshangaa Netanyahu kwa kusifia makombora mapya ya Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali kitendo cha Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel cha kuonesha majivuno na kusifia makombora mapya ya utawala huo wa Kizayuni.

Katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter leo Jumanne, Mohammad Javad Zarif ameandika, "Mwanzo, Netanyahu alisimama pambizoni mwa kiwanda cha kuzalisha bomu la nyuklia na kuitishia Iran. Hii leo anajivuna na kusifu kwa kiburi makombora ambayo eti yana uwezo wa kufika pahala popote."

Dakta Zarif amesema mataifa ya Magharibi yalipiga makelele mengi hivi karibuni baada ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufanyia majaribio kombora lake jipya la balestiki.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Waziri Mkuu wa Israel aliingiwa na kiwewe kutokana na mafanikio hayo ya Tehran ya kuzalisha makombora ya kujihami, huku Wamagharibi nao pia wakimuiga Netanyahu na kueleza eti 'wasiwasi wao' juu ya majaribio hayo ya makobora yaliyofanywa na Jamhuri ya Kiislamu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Hapo jana Netanyahu alidai kuwa utawala huo haramu unaunda makombora yenye uwezo wa kupiga sehemu yoyote katika eneo la Mashariki ya Kati.

Matamshi ya Netanyahu yametolewa siku chache baada ya Waziri Mkuu huyo wa Israel mwenye sera za kupenda vita na chokochoko kusema kuwa Tel Aviv iko tayari kufanya mashambulizi ndani ya ardhi ya Iran iwapo uhai wake utakuwa hatarini.

Tags