Hizbullah: Tumejitayarisha kukabiliana na hujuma tarajiwa ya utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i51339-hizbullah_tumejitayarisha_kukabiliana_na_hujuma_tarajiwa_ya_utawala_wa_kizayuni
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon amesisitiza kuwa wanamapambano wa muqawama wamejiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana na hujuma tarajiwa ya utawala haramu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 05, 2019 00:13 UTC
  • Hizbullah: Tumejitayarisha kukabiliana na hujuma tarajiwa ya utawala wa Kizayuni

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon amesisitiza kuwa wanamapambano wa muqawama wamejiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana na hujuma tarajiwa ya utawala haramu wa Israel.

Sheikh Naim Qassem amesema kuwa, mazingira tata yaliyopo hivi sasa katika eneo la Mashariki ya Kati, ni jambo lililo gumu kwa utawala wa Kizayuni kuacha kuanzisha vita vipya nchini Lebanon, lakini ametahadharisha kwamba iwapo Israel inataka kuanzisha vita hivyo, basi itambue kuwa, Hizbullah imejiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana na utawala huo khabithi. 

Naim Qassem, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah amesema kuwa Syria ndio njia kuu ya ardhini kwa uchumi wa Lebanon na kusisitiza kwamba, Harakati ya Hizbullah inafanya juhudi zake zote kwa ajili ya kuimarisha uhusiano kati ya Bairut na Damascus. Sheikhh Naim Qassem ameongeza kwamba, Wamarekani wanafanya njama za kuishawishi Lebanon iiwekee mashinikizo Syria kupitia faili la wakimbizi wa nchi hiyo sambamba na kuufanya kuwa mzito mwenendo wa kurejea wakimbizi hao nchini kwao.