Wanamgambo wa Kikurdi wa Syria wanatumia maelfu ya shule kama makao ya kijeshi
(last modified Fri, 27 Sep 2019 02:39:18 GMT )
Sep 27, 2019 02:39 UTC
  • Wanamgambo wa Kikurdi wa Syria wanatumia maelfu ya shule kama makao ya kijeshi

Wanamgambo wa Kikurdi kwa jina la Vikosi vya Kidemokrasia vya Syria wanaoungwa mkono na Marekani hadi kufikia sasa wamefunga shule zaidi ya elfu mbili katika mkoa wa Hasaka. Aidha wamezigeuza baadhi ya shule hizo kuwa makao yao ya kijeshi.

Wanamgambo hao wa Kikurdi wameamua kuzifunga shule hizo huko Hasakah na Qamishli kaskazini mashariki mwa Syria kwa sababu wakazi wa maeneo hayo hawaafiki watoto wao kufundishwa kwa mujibu wa mitaala ya masomo ya wanamgambo hao. 

Shule ya Amal Assyrian Elementary ni miongoni mwa shule zilizofungwa na wanamgambo wa Kikurdi huko Hasaka, Syria
 

Mamluki hao wenye mfungamano na Marekani hivi karibuni walizifunga pia shule za upili za serikali ya Syria katika mji wa Ras al Ain kaskazini mwa Hasakah; na kuzibadili pia shule za ufundi katika mji huo kuwa makao yao ya kijeshi. 

Wakazi wa maeneo ya kaskazini na kaskazini mashariki mwa Syria hadi kufikia sasa wameshafanya maandamano mengi kama radiamali kwa ukandamizaji na uvamizi wa wanamgambo hao wa Kikurdi.  

Tags