Misafara mitatu ya jeshi la kigaidi la Marekani yashambuliwa nchini Iraq
(last modified Sat, 26 Dec 2020 02:41:46 GMT )
Dec 26, 2020 02:41 UTC
  • Misafara mitatu ya jeshi la kigaidi la Marekani yashambuliwa nchini Iraq

Duru za kiusalama nchini Iraq zimeripoti kuwa misafara mingine mitatu ya jeshi la kigaidi la Marekani imeshambuliwa katika maeneo ya Dhi Qar, Diwaniya na Babil.

Kwa mujibu kanali ya habari ya Sabirin News, duru za kiusalama za Iraq zimetangaza kuwa, ulitokea mripuko wa bomu hapo jana katika njia uliopita msafara uliobeba zana na vifaa kwa ajili ya jeshi la Marekani katika eneo la Diwaniya mkoani Al-Qadisiyyah. Dereva mmoja alijeruhiwa na magari ya msafara huo yaliharibiwa.

Duru hizo zimeongeza kuwa, mripuko mwingine wa bomu ulitokea katika njia uliyopita msafara mwingine wa jeshi la kigaidi la Marekani katika eneo moja la mkoa wa Dhi Qar kusini mwa Iraq.

Kwa mujibu wa duru hizo, msafara mwingine wa tatu wa jeshi vamizi la Marekani ulishambuliwa jana hiyo hiyo katika mkoa wa Babil kusini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad, ambao ulipelekea vikosi vya utoaji misaada kutumia saa kadhaa hadi kufanikiwa kuzima moto uliosababishwa na mripuko wa bomu uliolenga msafara huo wa jeshi hilo la kigaidi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kundi la Qas'im al-Jabbarin limetangaza kuwa ndilo lililohusika na mashambulio hayo.

Askari wa jeshi la kigaidi la Marekani wakiranda katika mitaa ya Iraq

Kabla ya mashambulio hayo matatu, asubuhi ya jana Ijumaa pia msafara mwengine wa jeshi la Marekani ulishambuliwa kwa bomu lililotegwa kando ya barabara  katika eneo la As-Samawah mkoani Muthanna kusini mwa Iraq.

Katika miezi ya karibuni, mashambulio yanayofanana ya miripuko ya mabomu yamekuwa yakilenga misafara ya jeshi la kigaidi la Marekani nchini Iraq.

Wananchi na makundi mbalimbali ya Kiiraqi yanataka askari wa jeshi la kigaidi la Marekani waondoke nchini humo ikizingatiwa kuwa mnamo tarehe 5 Januari 2020 bunge la Iraq lilipitisha mpango kuhusiana na askari hao kuondoka katika ardhi ya nchi hiyo.../

 

 

Tags