Wamarekani waendelea kuiba mafuta na maliasili ya Syria
(last modified 2021-07-04T02:36:32+00:00 )
Jul 04, 2021 02:36 UTC
  • Wamarekani waendelea kuiba mafuta na maliasili ya Syria

Wanajeshi vamizi na maharamia wa Marekani wanaendelea kuiba mafuta ya nchi ya Syria waliyoivamia kinyume cha sheria na kuhamisha nishati hiyo nje ya mipaka ya Syria kupitia kaskazini mwa Iraq.

Hayo yamefichuliwa na shirika la habari la SANA ambalo limezinukuu duru za kieneo katika kijiji cha al Suwayda zikisema jana Jumamosi kwamba, msafara wa jeshi vamizi la Marekani wenye malori 37 ya mafuta ya Syria uumevuka mpaka wa nchi hiyo na kuingia Iraq.

Duru hiyo imeongeza kuwa, magari kadhaa ya kijeshi yaliyojizatiti kwa silaha nzito ya wanajeshi magaidi wa Marekani yameongozana na msafara huo.

Baadhi ya vibaraka waliorubuniwa na mabeberu wanasaidiana na wanajeshi vamizi wa Marekani kuiba kiwango kikubwa cha mafuta ya Syria kila siku ya kuyasafirisha nje ya nchi hiyio kupitia mpaka wake na Iraq. 

Msafara wa wanajeshi maharamia wa Marekani katika ardhi ya wananchi wa Syria

 

Viongozi wa Syria mara chungu nzima wamekuwa wakiishitaki Marekani kwa Umoja wa Mataifa na vyombo vinavyodai kutetea haki za mataifa mengine duniani, lakini hakuna hatua inayochukuliwa.

Siku chache zilizopita pia Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Russia alisema kuwa, Marekani inaendelea kuiba mafuta na ngano ya Syria. Sergei Vershinin alikiambia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichojadili hali ya Syria kwamba, misafara ya wanajeshi wa Marekani kila siku inaiba na kutorosha mafuta na ngano inayozalishwa nchini Syria na kuipeleka Iraq.  

Aliongeza kuwa, Wamarekani wanaendelea kuiba na kufanya magendo ya mafuta na ngano ya Syria huku watu wa Syria wenyewe wakisumbuliwa na uhaba wa chakula na nishati.

Tags