Jeshi la Syria latungua makombora ya utawala haramu wa Israeli
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i75588-jeshi_la_syria_latungua_makombora_ya_utawala_haramu_wa_israeli
Mfumo wa ngao ya makombora wa Syria umefanikiwa kutungua aghalabu ya makombora ya Israeli yaliyokuwa yamevurumishwa kuelekea kwenye mkoa wa Homs, katikati mwa nchi hiyo ya Kiarabu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 10, 2021 04:17 UTC
  • Jeshi la Syria latungua makombora ya utawala haramu wa Israeli

Mfumo wa ngao ya makombora wa Syria umefanikiwa kutungua aghalabu ya makombora ya Israeli yaliyokuwa yamevurumishwa kuelekea kwenye mkoa wa Homs, katikati mwa nchi hiyo ya Kiarabu.

Vadim Kulit, naibu mkuu wa Kituo cha Maridhiano cha Russia kwa ajili ya  Syria ametoa taarifa hiyo na kuongeza kuwa, mfumo wa makombora ya angani wa Pantsir, ulitumiwa na Jeshi la Syria katika kutungua makombora 8 kati ya 12 yalivyorumishwa na Wazayuni siku ya Ijumaa.

Ameongeza kuwa, aghalabu ya makombora hayo yaliyovurumishwa na jeshi la utawala haramu wa Israel yalitunguliwa yakiwa angani na hivyo hayakuweza kulenga yalikokosudiwa.

Hata hivyo, Kulit amesema shambulio hilo la kichokozi la Israel limepelekea kujeruhiwa wanajeshi sita wa Syria, mbali na kulisababisha hasara kidogo jeshi la nchi hiyo ya Kiarabu.

Ngao ya makombora ya Syria

Mapema mwezi uliopita, ndege nne za kivita za Jeshi la Anga la Israeli aina ya F-15 zilivurumisha makombora 24 yaliyolenga Jamhuri ya Kiarabu ya Siria kutoka anga ya Lebanon, lakini mfumo wa ulinzi wa anga wa Jeshi la Syria ulitungua 21 kati yao.

Mara kwa mara, Syria imekuwa ikilaani mashambulio ya utawala wa Israeli katika ardhi yake ikisema vitendo hivyo vya uchokozi vya Tel Aviv havitaathiri azma ya nchi hiyo ya Kiarabu katika vita dhidi ya ugaidi.