Nasrullah akanusha madai ya kuwepo vikosi vya Hizbullah nchini Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i81562-nasrullah_akanusha_madai_ya_kuwepo_vikosi_vya_hizbullah_nchini_ukraine
Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amekanusha vikali ripoti ya baadhi ya vyombo vya habari inayodai kuwa wapiganaji kadhaa na washauri wa kijeshi wa harakati hiyo ya muqawama wapo Ukraine kupigana katika safu moja na wananajeshi wa Russia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 19, 2022 08:55 UTC
  • Nasrullah akanusha madai ya kuwepo vikosi vya Hizbullah nchini Ukraine

Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amekanusha vikali ripoti ya baadhi ya vyombo vya habari inayodai kuwa wapiganaji kadhaa na washauri wa kijeshi wa harakati hiyo ya muqawama wapo Ukraine kupigana katika safu moja na wananajeshi wa Russia.

Sayyid Hassan Nasrullah alisema hayo jana Ijumaa katika hotuba yake aliyoitoa kwa mnsaba wa Maadhimisho ya Siku ya Maskauti wa Al-Mahdi na kueleza kuwa, vyombo vya habari vya Waarabu vimeeneza uvumi huo kwa kunukuu duru za kijeshi za Ukraine.

Sayyid Nasrullah amenukuliwa na televisheni ya al-Manar akisisitiza kuwa, "Nakadhibisha vikali uvumi wa namna hii. Huu ni urongo na uvumi usio na msingi wowote. Hizbullah haijatuma wapiganaji au wataalamu wowote Ukraine."

Mgogoro wa Ukraine

Hivi karibuni pia, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon alisisitiza kuwa, mgogoro wa Ukraine umedhihirisha wazi undumakuwili na mmomonyoko wa kimaadili wa Wamagharibi.

Kwengineko katika hotuba yake ya jana Ijumaa, Sayyid Hassan Nasrullah ametoa mwito kwa serikali ya Lebanon kuunda kamati ya dharura ya kuchunguza athari za kiuchumi kutokana na mgogoro wa Ukraine, hususan suala la bei za bidhaa muhimu.