-
Wanajeshi wa Kizayuni waangamizwa Gaza na wanamuqawama wa HAMAS
Oct 14, 2024 08:07Wanajeshi kadhaa wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameangamizwa na kujeruhiwa na Mujahidina wa Brigedi za Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) kusini mwa Ukanda wa Gaza.
-
Israel yateketeza mahema kwenye Hospitali ya Ghaza na kuwachoma moto Wapalestina wakiwa hai
Oct 14, 2024 02:42Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeishambulia kwa mabomu kambi ya wakimbizi katika eneo la kati la Ukanda wa Ghaza na kusababisha moto mkubwa uliopelekea kuuawa shahidi Wapalestina waliokuwa wametafuta hifadhi kwenye eneo hilo kutokana na hilaki ya vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na utawala huo ghasibu.
-
Hizbullah: Israel imemimina mabomu yaliyopigwa marufuku ya vishada kusini mwa Lebanon
Oct 14, 2024 02:12Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah imesema utawala wa Kizayuni wa Israel umemimina "makombora yaliyosheheni mabomu ya vishada" kwenye vitongoji vya kusini mwa Lebanon.
-
Makumi ya wanajeshi wa Israel wauawa, kujeruhiwa; Hizbullah yapiga kambi ya jeshi huko Haifa
Oct 13, 2024 23:51Mujahidina wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon wamefanya mashambulizi makali dhidi ya vituo vya kijeshi na maeneo ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Haifa, na kuua wanajeshi kadhaa wa utawala huo.
-
Wanajeshi wa Kizayuni waangamizwa kusini mwa Lebanon
Oct 13, 2024 23:07Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon jana ilikabiliana vikali na wanajeshi wa kizayuni na kuishambulia kambi muhimu ya Israel huko kusini mwa nchi hiyo.
-
WHO: Nusu ya vituo vya tiba vya Lebanon havifanyi kazi kutokana na mashambulio ya Israel
Oct 13, 2024 22:52Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO amesema, mfumo wa huduma za afya wa Lebanon umeelemwa na mahitaji yanayoongezeka kutokana na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya nchi hiyo.
-
Israel yafanya maangamizi Lebanon, yateketeza msikiti na soko, idadi ya waliouawa na kujeruhiwa haijajulikana
Oct 13, 2024 07:27Msururu wa mashambulizi ya kinyama ya anga yaliyofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel yameteketeza kikamilifu msikiti na kubomoa soko kusini mwa Lebanon, katika kile kilichoelezewa kama "uangamizaji wa kila kitu" huku utawala huo ghasibu ukishadidisha na kupanua mashambulizi yake ya mabomu na makombora katika kila pembe ya nchi hiyo.
-
Hamas: Israel imeshindwa kusambaratisha muqawama
Oct 13, 2024 03:29Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (muqawama) Palestina, Hamas, imesema utawala wa haramu wa Israel umeshindwa kusambaratisha wanamuqawama shupavu katika Ukanda wa Gaza.
-
Hizbullah yashambulia Tel Aviv kwa ndege zisizo na rubani
Oct 13, 2024 03:19Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imetekeleza mashambulizi ya kulipiza kisasi katika viunga vya mji wa Tel Aviv ulio katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu kwa kutumia idadi kubwa ya ndege za kivita zisizo na rubani aina ya kamikaze.
-
Hamas: Mauaji ya Jabalia ni kulipiza kisasi dhidi ya raia wa Palestina
Oct 12, 2024 08:54Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika kukabiliana na jinai mpya iliyofanywa na utawala wa Kizayuni katika kambi ya Jabalia, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, imetoa taarifa na kueleza kuwa, mauaji ya utawala huo ghasibu katika kambi hiyo ni kuwaadhibu wakazi wa eneo kwa kusimama kidete na kupinga juhudi za utawala wa Kizayuni za kuwafukuza Wapalestina katika ardhi zao.