Bunge la Ulaya: Uingereza ianze mchakato wa kuondoka EU
Spika kwa Bunge la Ulaya ametaka kuanza mchakato wa kuondoka Uingereza katika Umoja wa Ulaya.
Martin Schulz Spika wa Bunge la Ulaya amemtaka David Cameron Waziri Mkuu wa Uingereza aanze mchakato wa kuiondoa nchi hiyo katika Umoja wa Ulaya kuanzia Jumanne wiki hii.
Spika wa Bunge la Ulaya ameeleza kuwa kuna wasiwasi kwamba hatua hiyo ya Uingereza itasababisha ukosefu wa utulivu na soko la ajira kuwa hatarini.
Martin Schulz amesema wanataraji kuwa serikali ya Uingereza itatekeleza ahadi zake kuanzia sasa.
Vyama vinne vikuu katika bunge la Ulaya pia vimeandaa rasimu na kumtakak David Cameron aanze mchakato wa kuondoka nchi hiyo katika Umoja wa Ulaya kuanzia Jumanne wiki hii.
Kikao cha Marais na Mawaziri Wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kitakachochunguza kura ya maoni kuhusu kujiondoa Uingereza ndani ya Umoja wa Ulaya kimepangwa kufanyika Jumanne wiki hii huko Brussels mji mkuu wa Ubelgiji.