Nov 01, 2023 08:09 UTC
  • Kremlin: Kuanzisha chombo bora badala ya Baraza la Usalama la UN kunahitaji mwafaka wa kimataifa

Msemaji wa Ofisi ya Rais wa Russia amekiri kwamba, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kutekeleza majukumu yake. Dmitry Peskov ameyasema hayo akijadili fikra zilizopendekezwa kuhusu udharura wa kuanzishwa taasisi yenye ufanisi badala ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la TASS, Dmitry Peskov, msemaji wa Ofisi ya Rais wa Russiai, amesema kuwa kuanzishwa taasisi hiyo ufanisi badala ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kunahitaji makubaliano ya kimataifa.

Msemaji wa Rais wa Russia pia amesema kuwa siku zijazo tu ndizo zitakazoonyesha ikiwa inawezekana kufikia maelewano kama haya katika nyakati hizi ngumu na maoni tofauti.

Dmitry Peskov ameongeza kuwa, licha ya kukosekana kwa ufanisi wa kutatua masuala mengi katika ajenda ya kimataifa, Russia bado inauona mfumo wa Umoja wa Mataifa kama utaratibu wa kimataifa usioweza kubadilishwa na ambao kwa sasa hakuna mbadala wake unaofaa.

Hapo awali, msemaji wa Ofisi ya Rais wa Uturuki alisema kuwa kuna haja ya kuunda mashirika mapya ya kimataifa ambayo yatakuwa mbadala wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa sababu baraza hilo halina uwezo tena wa kutatua masuala ya kimataifa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataiifa

Wito wa kuundwa taasisi na jumuiya mbadala wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unashika kasi zaidi katika kipindi cha sasa ambapo Umoja wa Mataifa umeshindwa kuchukua maamuzi muhimu ya kusitisha mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala katili wa Israel ukisaidiwa kwa hali na mali na mataifa ya Magharibi hususan Marekani dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza huko Palestina. 

Karibu watu elfu tisa wamekwishauawa shahidi hadi sasa katika mashambulizi ya kinyama ya Israel. 

Tags