Jan 14, 2024 02:43 UTC
  • Hatua za undumakuwili za nchi za Ulaya kuhusu ugaidi

Mahakama ya Rufaa ya Denmark inayojulikana kwa jina la "The Eastern High Court" Ijumaa tarehe 12 Januari ilipasisha hukumu ya kifungo jela kwa watu watatu ambao ni wanachama wa kundi linalotaka kujitenga la "Al Ahwaziya" ambao walituhumiwa kueneza ugaidi nchini na kukusanya taarifa za kijasusi kwa ajii ya Shirika la ujasusi la Saudi Arabia.

Mwaka 2022 mahakama ya chini  ya Denmark iliwahukumu watu hao watatu vifungo vya jela vya miaka sita, saba na nane kwa utaratibu. 

Katika upande mwingine, mahakama hiyo yya The Eastern High Court pia imepasisha hukumu iliyotolewa mwezi Februari mwaka juzi dhidi ya watu hao watatu kwa kosa la kujikusanya fedha za kufadhili hujuma za kigaidi kupitia kupokea krona milioni 5 ambazo ni sawa na dola milioni mbili na laki mbili, na kufanya juhudi za kujipatia kiasi cha krona milioni 15 nyingine kutoka Saudi Arabia kwa ajili ya kundi hilo linalotaka kujitenga.  

Kabla ya hapo, yaani Jumanne iliyopita Mahakama ya Rufaa ya Denmark au The Eastern High Court" iliidhinisha hukumu iliyotolewa na mahakama ya mwanzo kuhusu watuhumiwa hao watatu wanachama wa kundi la kigaidi la Al Ahwaziya kwa kueneza ugaidi na kuifanyia ujasusi Saudi Arabia. Mahakama hiyo imetangaza kuwa watu hao watatu walikuwa wakijihusisha na kukusanya taarifa kuhusu shakhsiya na taasisi mbalimbali nchini Denmark na nje ya nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na kkukusanya habari za kijasusi kuhusu masuala ya kijeshi ya Iran na kisha kutoa taarifa hizo kwa mashirika ya kijasusi ya Saudia. Kwa mujibu wa sheria za Denmark, adhabu ya watu hawa ilikuwa kwa uchache kifungo cha miaka 12 jela. Mahakama hiyo ya Eastern High Court ya Copenhagen iliamua kuwa wanachama hao watatu wa kundi la Al Ahwaziya wafukuzwe Denmark. Watu hao watatu watatumikia vifungo vyao katika magereza ya Denmark, lakini bado haijafahamika lini watafukuzwa nchini humo.

Mahakama ya Rufaa au Eastern High Court ya Copenhagen

Kama alivyobainisha Finn Borch Andersen, Mkuu wa Idara ya Ujasusi ya Denmark, watu hawa watatu wamekuwa wakiifanyia ujasusi Saudi Arabia tangu 2012. Watu hao wanaotajwa kuwa wanachama wa kundi la Al Ahwaziya ambao majina yao hayajatajwa, walitiwa nguvuni Februari mwaka 2020 katika mji wa Ringsted umbali wa kilomita 60 kusini magharibi mwa Copenhagen. Tuhuma zilizowakabili kuhusu kueneza ugaidi zilithibitishwa baada ya shambulizi la kigaidi la Septemba 22 mwaka 2018 dhidi ya gwaride la jeshi huko Ahwaz, kusini mwa Iran. 

Kundi la kigaidi la Al Ahwaziya katika miaka ya karibuni limetekeleza hujuma nyingi za kigaidi kwa lengo la kuibua machafuko na hali ya machafukoge katika mkkoa wa Khuzistan kusini mwa Iran; na linataka kuandaa mazingira ya kujitenga Khuzistan na Iran kupitia njia ya kuyumbisha hali ya usalama; hatua ambayo utawala wa dikteta wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein, ulifanya kila uwezalo ili kukifanikisha kwa kuanzisha mashambulizi dhidi ya Iran lakini uligonga mwamba. Kundi hili limehusika katika miripuko mingi ya mabomu ikiwemo mashambulizi katika ofisi ya gavana wa Ahwaz, kuripua visima na taasisi za mafuta.

Moja ya jinai kubwa sana iliyofanywa na kundi la kigaidi la Al Ahwaziya ni shambulio lililotekelezwa na wanachama wake wakati wa gwaride la vikosi vya ulinzi vya Iran huko Ahwaz, Septemba 22 mwaka 2018, ambapo watu wasiopungua 25, raia wa kawaida na wanajeshi, waliwauwa shahidi na wengine karibu 70 walijeruhiwa kwa kumiminiwa risasi. Baada ya shambulio hilo, kundi la al Ahwaziya lilitangaza waziwazi katika televisheni ya al Arabiyya inayomilikiwa na Saudi Arabia kuwa ndilo lililohusika na hujuma hiyo ya Ahwaz. Telavisheni hiyo ya Saudia haikutaja shambulio hilo huko Ahwaz nchini Iran kuwa ni hujuma ya kigaidi bali ililitaja kuwa ni shambulilo la watu "wenye silaha". Nchi za Ulaya ambazo zimewapa hifadhi viongozi na wanachama wa kundi hilo yaani  Denmark, Sweden na Uholanzi, hazikulaani hata kidogo hujuma hiyo ya kigaidi au kuchukua hatua ya kuwatia nguvuni viongozi na wanachama wa kundi hilo la kigaidi.  Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ililalamikia vikali suala hilo ambapo Bahram Qassimi, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran wa wakati huo alisema kuwa: "Ni jambo lisilokubalika kuona Umoja wa Ulaya hauyataji magenge kama haya kuwa ni ya kigaidi madhali hayajatekeleza operesheni za kigaidi katika ardhi za Ulaya."

Hjuma ya kigaidi mkoani Ahwaz mwaka 2018 

Hata hivyo nchi za Ulaya ziliamua kuwatia nguvuni na kuwafungulia mashataka wanachama wa kundi la Ahwaziya baada ya kuibuliwa suala la usalama wa taifa wa baadhi ya nchi za Ulaya kama Denmark, kufuatia wanachama kundi hilo kufanya ujasusi kwa manufaa ya Saudi Arabia. 

Japokuwa suala ugaidi limekuwa tatizo kuu kwa aghalabu ya nchi katika miaka ya karibuni, lakini nchi za Ulaya zimemechukua misimamo na hatua za undumakuwili katika kukabiloana na wa taizo hili ovu. Mfano wa wazi ni hatua za kinafiki na kindumakuwili za nchi za Ulaya katika kuamiliana na kundi la kigaidi la Al Ahwaziya; ambalo limefanya hujuma nyingi za kigaidi nchini Iran. Nchi za Ulaya hunyamaza kimya na kupuuza wakati kundi hili la kigaidi linapotekeleza hujuma za kigaidi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuruhusu kuendelea kutekelezwa hujuma za kundi hilo bila kizuizi chochote. Hata hivyo huchukua hatua pale hatua na vitendo vya kundi la Al Ahwaziya vinapokiuka na kwenda kinyume na maslahi, manufaa na usalama wa taifa wa nchi hizo. 

Katika muktadha huo, uungaji mkono wa muda mrefu wa baadhi ya nchi za Ulaya hususan Ufaransa kwa kundi la kigaidi la MKO umetia doa jeusi taswira ya nchi hizo hizo kutokana na hatua yao ya kutoa himaya kwa ugaidi kuwa sababu tu ya upinzani wa kundi hilo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.  Hii ni licha ya kwamba serikali za nchi za Ulaya zifahamu kikamilifu jinai kubwa zinazofanywa na kundi hilo dhidi ya wananchi wa Iran na Iraq lakini bado kundi la MKO linaendelea kuungwa mkono waziwazi na kwa siri na Paris katika harakati, hafla na mikutano yake mbalimbali. 

Tags