Mwendesha Mastaka Mkuu wa New York amfungulia mashtaka Trump na watoto wake
(last modified Fri, 15 Jun 2018 05:00:49 GMT )
Jun 15, 2018 05:00 UTC
  • Mwendesha Mastaka Mkuu wa New York amfungulia mashtaka Trump na watoto wake

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa New York nchini Marekani amemfungulia mashtaka Rais Donald Trump na watoto wake kutokana na shughuli zilizo kinyume cha sheria za taasisi ya misaada ya 'Donald J. Charity Foundation.'

Televisheni ya CNBC imeripoti kwamba, Barrow Androwood alimfungulia mashitaka Trump, watoto wake watatu na taasisi moja ya misaada ya rais huyo wa Marekani.  Mwendesha mashtaka mkuu wa mji wa New York amechukua hatua hiyo kutokana na shughuli za zaidi ya muongo mmoja za taasisi hiyo. Androwood pia ameituhumu taasisi hiyo kuwa inahusika na masuala ya kisiasa hususan katika kampeni za uchaguzi mkuu uliopita nchini humo.

Rais Donald Trump wa Marekani

Amesema kuwa, taasisi hiyo iliyosajiliwa kwa ajili ya shughuli za kimisaada, kwa mara kadhaa imehusika na miamala yenye lengo la kumnufaisha zaidi Trump na mashirika yake  sambamba na kukiuka sheria za taasisi za namna hiyo. Mbali na Rais Donald Trump, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa New York amemshitaki Donald John Trump Jr, mtoto mkubwa wa rais huyo, Eric Trump, mtoto mwingine wa kiume wa Trump ambaye pia ni mfanyabiashara na Ivanka Trump, mtoto wa kike wa rais huyo wa Marekani. Katika faili hilo, Androwood anataka kuitoza taasisi hiyo kiasi cha Dola milioni 2.8 kutokana na hasara ambayo zimesababishwa na shughuli zilizo kinyume na sheria za taasisi tajwa.

Tags