Maaskofu wa New York wasailiwa kutokana na kashfa ya ukatili wa kingono
(last modified Fri, 07 Sep 2018 08:17:04 GMT )
Sep 07, 2018 08:17 UTC
  • Maaskofu wa New York wasailiwa kutokana na kashfa ya ukatili wa kingono

Mwendesha Mashtaka wa New York nchini Marekani amewaita maaskofu wote wakuu wa jimbo hilo kwenda kwake kutokana na ukatili na udhlilishaji wa kingono uliofanywa na viongozi Kanisa Katoliki.

Barbara Underwood amewaita viongozi wa Kanisa Katoliki katika fremu ya uchunguzi anaofanyika kuhusu ukatili na udhlilishaji wa kingono wa makasisi wa kanisa hilo dhidi ya watoto wadogo.

Inaelezwa kwamba lengo la mwendesha mashtaka wa New York ni kutaka kujua msimamo wa kanisa hilo kuhusiana na suala hilo. Kabla ya hapo pia mwendesha mashtaka wa jimbo la Pennsylvania nchini Marekani, alitoa ripoti ya udhalilishaji wa kingono na ubakaji wa mamia ya makasisi wa Kanisa Katoliki dhidi ya maelfu ya watoto wadogo nchini humo.

Barbara Underwood, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Ney York aliyewaita maaskofu wa jimbo hilo

Taarifa zinasema vitendo hivyo vichafu vilifanywa katika vituo sita vya jimbo la Pennsylvania na maeneo mengine ya sira ya viongozi wa ngazi ya juu wa kanisa Katoliki. Katika miaka ya hivi karibuni Kanisa Katoliki limeendelea kuandamwa na kashfa za ufisadi wa kimaadili wa viongozi wake kutokana na kuhusishwa na udhalilishaji wa kingono. Kutokana na hali hiyo, hivi karibuni Katika moja ya hotuba zake, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis aliomba msamaha kwa makosa na uhalifuu waliofanyiwa wafuasi wa kanisa hilo kwa kusema, hakuna mtuanayeweza kunyamazia kimya matukio ya watu waliodhalilishwa, waliotekwa nyara bila hatia na kubakia na kovu na kumbukumbu chungu sana kutoka kwa viongozi wa kanisa.

Tags