Kulegeza msimamo Trump kuhusiana na Syria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i50617-kulegeza_msimamo_trump_kuhusiana_na_syria
Baada ya kupita miaka saba tangu Syria ikumbwe na mgogoro uliosababishwa na uingiliaji wa Marekani pamoja na waitifaki wake wa Ulaya wa Kiarabu katika masuala ya ndani ya nchi hiyo kwa kuyaunga mkono makundi ya kigaidi ili kuipindua serikali halali ya nchi hiyo; hivi sasa mlingano wa nguvu umebadilika kikamilifu kwa maslahi ya serikali ya Syria na waitifaki wake.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jan 03, 2019 22:55 UTC
  • Kulegeza msimamo Trump kuhusiana na Syria

Baada ya kupita miaka saba tangu Syria ikumbwe na mgogoro uliosababishwa na uingiliaji wa Marekani pamoja na waitifaki wake wa Ulaya wa Kiarabu katika masuala ya ndani ya nchi hiyo kwa kuyaunga mkono makundi ya kigaidi ili kuipindua serikali halali ya nchi hiyo; hivi sasa mlingano wa nguvu umebadilika kikamilifu kwa maslahi ya serikali ya Syria na waitifaki wake.

Marekani hivi sasa ina taathira ya kiwango cha chini katika masuala yanayojiri huko Syria huku mlingano wa nguvu ukibadilika na kuwa kwa maslahi ya makundi ya kigaidi. Wakati huo gharama kubwa za kuweko wanajeshi wa Marekani huko Syria na muhimu kuliko yote hatua ya Rais Donald Trump ya kupunguza uwepo wa Washington katika eneo imempelekea rais huyo kuchukua uamuzi wa ghafla tarehe 19 mwezi huu na kutangaza kuwaondoa wanajeshi wa Marekani waliopo Syria. 

Rais wa Marekani amedai kuwa baada ya kupatikana ushindi dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh hakuna sababu ya kuendelea kubaki huko Syria. Pamoja na hilo, inaonekana kuwa Trump yuko chini ya mashinikizo makubwa ya ndani na vilevile ya waitifaki wa Ulaya wa Washington  ambapo hivi sasa amelazimika kulegeza msimamo wake mkuu kuhusu Damascus kwa kubadilisha  mipango yake ya awali ambapo ameongeza muda wa kuondoka wanajeshi wa Marekani waliopo Syria hadi siku 120 badala ya 30. Kuhusiana na suala hilo, Trump juzi Jumatano tarehe Pili Januari alidai akiwa ndani ya ikulu ya Marekani (White House) kuwa Marekani itaendelea kuwalinda Wakurdi licha ya wanajeshi wa nchi hiyo kuondoka huko Syria. 

wapiganaji wai Kikurdi wa nchini Syria 

Hii ni katika hali ambayo kabla ya hapo Trump alidai kuwa haoni tena sababu ya kuendelea kuwepo nchini Syria wanajeshi wa Marekani sambamba na kutangaza kupatikana ushindi dhidi ya Daesh na wakati huo huo akitilia mkazo ulazima wa kutekelezwa jukumu jingine yaani kuwaunga mkono wapiganaji wa Kikurdi wa Syria. Suala hilo linaonyesha namna Trump asivyo na ufahamu wowote sahihi kuhusu yanayojiri katika medani na wala kuhusu hali waliyo nayo wanajeshi wa Marekani huko Syria na vilevile vikosi waitifaki wao yaani wanamgambo wa Kikurdi na wale wanaojulikana kama vikosi vya kidemokrasia vya Syria.  

Miaka kadhaa iliyopita, Washington ilituma wanajeshi wake katika maeneo ya kaskazini na kaskazini mashariki mwa Syria wakiwa pamoja na wanamgambo wa Kikurdi na vikosi vya kidemokrasia vya Syria na kudai kuwa eti inaendesha mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh. Pamoja na hayo yote, kuondoka wanajeshi wa Marekani huko Syria ni suala lililowashtua waitifaki wa Washington. Waitifaki hao wa Marekani wamelazimika kuliomba jeshi la Syria liingie katika baadhi ya maeneo yanayodhibitiwa na Wakurdi ukiwemo mji wa Manbij na maeneo ya kandokando yake ili kuzuia tishio la kushambuliwa na Uturuki. 

Gazeti la New York Times liliandika katika uchambuzi wake wa tarehe 19 mwezi uliopita wa Disemba kwamba: Kuondoka Marekani huko Syria kutakuwa  moja ya kufeli kwa wapiganaji wa Kikurdi.   

Kuendelea uungaji mkono huo kwa wapiganaji wa Kikurdi ni moja ya matakwa ya waitifaki wa Ulaya wa Washington. Kuhusiana na suala hilo, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa Jumatano wiki hii alifanya mazungumzo ya simu ya Rais Vladimir Putin wa Russia na kusisitizia ulazima wa kulindwa vikosi vya muungano wa pamoja huko Syria hususan wapiganaji wa Kikurdi.  

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa 

Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Elize imeeleza kuwa: Rais wa Ufaransa amesisitizia ulazima wa kutambuliwa haki za wenyeji na kulinda vikosi vya muungano wa pamoja hususan Wakurdi kwa kuzingatia majukumu yao katika mapambano dhidi ya ugaidi. 

Wakosoaji kwa upande wao wanaona kuwa uamuzi wa Trump wa kuondoa wanajeshi wa Marekani nchini Syria ni kusalimu amri kikamilifu; ni msimamo ambao ameuchukua bila ya kuchunguza na kutilia maanani taathira zinazoweza kujitokeza kufuatia uamuzi huo na kwamba hatua hiyo itakuwa na athari kubwa mbaya kwa Washington na waitifaki wake. Jambo hilo   limempelekea Trump katika msimamo wake mwingine kusisitiza juu ya uwezekano wa kutekelezwa oparesheni huko Syria licha ya kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini humo. 

Kiujumla tunaweza kusema kuwa, serikali ya Trump imewaondoa tu wanajeshi wake nchini humo na kuwahamishia nchini Iraq badala ya kuwaondoa kikamilifu na kwa pande zote huko Syria na itaendelea kujiweka tayari kwa ajili ya  ya uingiliaji wowote wa kijeshi unaoweza kujiri huko Syria.