Maandamano ya kupinga safari ya Meya wa Israel mjini Paris, Ufaransa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i54484-maandamano_ya_kupinga_safari_ya_meya_wa_israel_mjini_paris_ufaransa
Wanaharakati na watetezi wa haki za Wapalestina nchini Ufaransa wamefanya maandamano ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina katika mji mkuu wa nchi hiyo Paris, sambamba na kulaani safari ya Meya wa Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel, nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 01, 2019 08:08 UTC
  • Maandamano ya kupinga safari ya Meya wa Israel mjini Paris, Ufaransa

Wanaharakati na watetezi wa haki za Wapalestina nchini Ufaransa wamefanya maandamano ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina katika mji mkuu wa nchi hiyo Paris, sambamba na kulaani safari ya Meya wa Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel, nchini humo.

Meya huyo wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Moshe Leon alikuwa ameenda Paris kwa ajili ya kuhudhuria sherehe iliyofanyika jana Jumapili ya kuuita moja ya mizunguko mikubwa ya Paris 'Medani ya Jerusalem'. 

Mbali na kubeba bendera za Palestina, waandamanaji hao walikuwa wamebeba pia mabango yaliyokuwa na jumbe za kuwanga mkono Wapalestina.

Waandamanaji hao wamesikika wakimkashifu na kumshutumu Meya wa Paris, Annie Hidalgo, kwa kumualika nchini humo Meya wa Quds Tukufu inayokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.

Ubalozi wa Marekani mjini Quds

Olivia Zemor, rais wa vuguvugu la wananchi wa Ulaya wanaoiunga mkono Palestina kwa jina CAPJPO-Europalestine amesema Moshe Leon ni Mzayuni na mbaguzi wa kupindukia, ambaye yuko tayari kutumia muda na fedha zake kuhakikisha kuwa Wapalestina wote wametokomezwa.

Naye Nicolas Shahshahani, msemaji wa vuguvugu hilo amesema hatua hiyo ya kuuita mzunguko wa barabara ya Paris "Medani ya Jerusalem" ni kujaribu kubakisha hai picha ya Israel nchini Ufaransa, na kwamba kitendo hicho hakitofautiani na hatua ya Marekani ya kuuhamishia ubalozi wake mjini Quds kutoka Tel Aviv.