Umaarufu wa Donald Trump wazidi kuporomoka nchini Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i57351-umaarufu_wa_donald_trump_wazidi_kuporomoka_nchini_marekani
Uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani unaonesha kuwa, idadi kubwa zaidi ya Wamarekani hawamtaki rais wa nchi hiyo Donald Trump na wanaamini kwamba ni mkosa katika kashfa ya "Ukraine Gate."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 18, 2019 23:11 UTC
  • Umaarufu wa Donald Trump wazidi kuporomoka nchini Marekani

Uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani unaonesha kuwa, idadi kubwa zaidi ya Wamarekani hawamtaki rais wa nchi hiyo Donald Trump na wanaamini kwamba ni mkosa katika kashfa ya "Ukraine Gate."

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na APC News kwa kushirikiana na taasisi ya Ipsos yaliyotangazwa jana Jumatatu yanaonesha kuwa, asilimia 70 ya wananchi wa Marekani wanaamini kuwa Donald Trump ni mkosa katika kashfa ya kumtaka Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine afanye uchunguzi dhidi ya Joe Biden, mpinzani wa Trump katika uchaguzi wa rais wa 2020 wa nchini Marekani. 

Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi huo, asilimia 51 ya wananchi wa Marekani wanasema kuwa, si tu kwamba kitendo hicho cha Trump ni kosa, bali inabidi aitwe mbele ya bunge akajieleze na hatimaye ang'olewe madarakani.

Maandamano ya kupinga ukandamizaji nchini Marekani

 

Asilimia 25 tu ya watu walioshiriki kwenye uchunguzi huo wa maoni wanaamini kuwa, Trump hakufanya makosa katika kashfa ya "Ukraine Gate."

Umaarufu wa rais wa Marekani umeporomoka sana baada ya kuibuka kashfa ya "Ukraine Gate" ambapo iligundulika kwamba Donald Trump alizungumza kwa njia ya simu na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na kumtaka afanye uchunguzi kuhusu Joe Biden, mgombea urais wa 2020 nchini Marekani kama anataka White House iidhinishe msaada kwa Ukraine.

Wananchi wengi wa Marekani wanataka Baraza la Congress la nchi hiyo limuite Trump kujieleza na baadaye limpigie kura ya kumpokonya urais.