Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Marekani chaongezeka maradufu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i57863-kiwango_cha_ukosefu_wa_ajira_nchini_marekani_chaongezeka_maradufu
Wizara ya Kazi nchini Marekani imetoa ripoti mpya ikisema kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira nchini humo kimeongezeka kwa kiwango cha juu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 13, 2019 23:34 UTC
  • Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Marekani chaongezeka maradufu

Wizara ya Kazi nchini Marekani imetoa ripoti mpya ikisema kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira nchini humo kimeongezeka kwa kiwango cha juu.

Taarifa hiyo ya Wizara ya Kazi ya Marekani imeongeza kuwa, maombi ya awali ya bima ya watu wasiokuwa na kazi kufikia mwishoni mwa juma hili, yameongezeka kwa watu elfu 49, ikilinganishwa na maombi ya wiki iliyopita ambapo ni watu laki mbili na tatu tu ndio walikuwa kwenye orodha ya maombi hayo ya bima ya wasiokuwa na ajira. Imeendelea kubainisha kwamba kwa sasa kiwango hicho kimefikia watu laki mbili na elfu 52. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hiki ni kiwango cha juu zaidi cha maombi ya awali ya bima ya watu wasiokuwa na kazi, tokea tarehe 30 Disemba mwaka 2017.

Watu wasio na ajira nchini Marekani waongezeka

Ongezeko hilo la ukosefu wa kazi wiki nchini Marekani linajiri katika hali ambayo Ijumaa iliyopita Idara ya Takwimu ya Kazi nchini humo ilitoa ripoti ikiwanukuu viongozi wa serikali ya Marekani waliodai kuwa mwezi Novemba mwaka huu waliongeza fursa za kazi kwa ajili ya watu laki mbili na elfu 66. Aidha Wizara ya Kazi ya Marekani imesema kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira ndani ya nchi hiyo kimepungua kwa asilimia 3.5, kiwango ambacho ni kidogo zaidi katika kipindi cha karibu miongo mitano iliyopita.